Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Makete Mkoani Njombe ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya usimamizi wa mitihani Wiliam Makufwe amesema jumla ya watahiniwa wa darasa la saba 2,623 wanafanya mtihani Leo na kesho kwa maana tarehe 11 na 12 Septemba,2024 wilayani hapo

Amesema watahiniwa 2,623 kati yao wanaofanya mtihani kwa lugha ya kingereza ni 49 na 2,574 wanafanya kwa lugha ya kiswahili, watahiniwa hao wameganywa katika mikondo 144 na hii ni kutokana na jiografia ya wilaya ya Makete.

Akizungumza na mwandishi wetu amesema halamshauri ya wilaya ya Makete inasimamia mitihani hiyo kwa kuzingatia miongozo, taratibu, sheria za Baraza la mitihani Tanzania (Necta) Makufwe ameishukuru serikali inayongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha ufanyaji mitihani na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza sambamba na hilo amesema wanategemea matokeo mazuri kwani watoto wamefundishwa na kuandaliwa vizuri na wana ulewa wa kutosha

Baraza la mitihani Tanzania (Necta) kupitia kwa katibu mtendaji wa Baraza hilo DKt Said Mohammed amesema jumla ya watahiniwa 1,230,680 wanafanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi hapa nchini.

Share To:

Post A Comment: