Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg Juma Mussa Hokororo mapema hii Leo ametoa maelekezo kuhusu utaratibu Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Ikiwa ni Moja ya mchakato Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.
Aidha miongoni mwa maelekezo yaliyotolewa na ndg,Juma ni Pamoja na Siku ya Uchaguzi, Muda na sehemu yakuandikisha wapiga Kura, Muda na mahali pakufanyia Uchaguzi , Sifa za wanaostahiki kupiga na kugombea nafasi za Uongozi, Nafasi zinazogombewa Ndani ya Serikali za Mitaa, Siku ya utoaji na urejeshwaji wa Fomu za kugombea nafasi za Uongozi wa Serikali za Mitaa, Uteuzi wa Viongozi, Ukataji wa Rufaa, Siku na Utaratibu wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa,Aidha Juma Mussa Hokororo ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza katika kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Kwa kufuata kanuni na taratibu zilizotolewa ili kuhimiza maendeleo ya Halmashauri na Taifa Kwa Ujumla.
Post A Comment: