Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Tanzania (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kinga juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya kwa waumini wa dini ya kikristo 310 katika kambi ya Kisabato Sanawari 2024, jijini Arusha
Waumini hao wameelezwa kwa kina uhusiano wa afya ya akili na matumizi ya dawa za kulevya kwa kipindi cha mwezi Septemba 2024 wa kuhamasisha na kukuza uelewa wa jamii kuhusu kuzuia watu kujiua
Washiriki waliohudhuria kambi hiyo iliyofanyika Septemba 11.2024 wamehimizwa kutokuwanyanyapa waraibu wa dawa za kulevya badala yake wawaelekeze waraibu hao katika huduma za matibabu zilizopo karibu na mazingira wanayoishi.
Post A Comment: