Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) tarehe 18.09.2024 imetoa elimu kinga kwa jamii juu ya madhara ya tatizo la dawa za kulevya wilayani Siha Mkoa wa Kilimanjaro.
Jumla ya watu takribani 1,400 walipatiwa elimu hiyo ikihusisha madereva wa magari madogo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Namwai,Matadi na Askari wa Jeshi la Akiba la Mgambo pamoja na wananchi na wafanyabiashara wa Soko la Sanya Juu.
DCEA Kanda ya Kaskazini iliwahamasisha wananchi wa wilaya ya Siha washirikiane na Mamlaka katika mapambano dhidi ya tatizo la dawa za kulevya kwa kutoa taarifa za wahalifu wa dawa hizo wanaopatikana katika maeneo yao wanayoishi kwa kupiga namba ya simu ya bure ya 119.
Post A Comment: