Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mkoani Pwani Shaibu Ndemanga leo Septemba 11,2024 amekabidhi Ofisi kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva .


Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Lindi iliyopo Manispaa ya Lindi ikiwa ni baada ya hivi karibuni Rais Dkt.Samia Suluhu Hasan kuwahamisha vituo vya kazi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa Ofisi Mkuu wa Wilaya ya Lindi Victoria Mwanziva ameomba watumishi na wananchi wa Lindi wampokee na kumpa ushirikiano katika kutekeleza majukumu ya kuwatumikia wananchi.




Share To:

Post A Comment: