Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewahakikishia wakazi wa Mtaa wa Kipunguni kata ya Kipawa waliopisha ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Julius Kambarage Nyerere kuwa hadi kufikia Novemba watakakua wamelipwa fidia zao.

Hayo ameyabainisha Leo Septemba 13, 2024 wakati akiendelea na ziara yake ya kusikiliza na kutatua Kero za Wananchi wa Kata Za Kipawa, Kiwalani na Minazi Mirefu ambapo kwa wakazi wa Kata hizo changamoto kubwa waliyoiibua ni kutokulipwa fidia za Maeneo yao jambo linalowaletea ugumu katika kuendeleza maeneo hayo kwa kuboresha makazi yao.

Akizungumza na wananchi hao Mhe. Mpogolo amewataka wakazi hao kuwa wavumilivu kwani suala hilo linakwenda kupatiwa ufumbuzi kwa ukaribu na hadi kufikia Novemba 2024 wakazi hao  watakua washalipwa fidia zao.

Kipekee natoa Shukrani zangu za dhati  kwenu wana Kipunguni kwa uvumilivu na uzalendo mliouonyesha kwa Nchi yenu kwa kipindi chote mlichokua mkisubiria fidia hivyo Napenda kuwafahamisha kilio chenu cha muda mrefu Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amekisikia na ameshatoa maelekezo kwamba malipo yaanze kufanyika, kinachosubiriwa sasa ninamna Wataalamu wetu wanavyoandaa mfumo mzuri wa malipo hivyo Niwatie mono kwamba hadi kufikia mwezi Octoba mwishoni  mtakua mmelipwa fidia zenu”. Amesisitiza Mhe.Mpogolo.

Share To:

Post A Comment: