MKUU wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amemwelekeza Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elhuruma Mabelya, kuwasaka na kuwanasa wale wote waliokopa jumla ya Sh. bilioni 17 katika halmashauri hiyo na kushindwa kurejesha.


Amesema fedha hizo ni zilizo kuwa zikitolewa kwa wajasiriamali kupitia mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu.

Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata za Mnyamani, Vingunguti na Buguruni.

“Hizi sh.bilioni 17 halmashauri iliwakopesha watu lakini hawajarejesha mpaka sasa.Ziko katika mzunguko,”alisema.

Amemtaka mkurugenzi huyo kuangalia utaratibu wa kuwatafuta na kuwapata wahusika na kuchukua hatua.
Share To:

Post A Comment: