Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo leo Septemba 12 ,2024 ameendelea na ziara ya kutatua kero za Wananchi wa Kata za Kitunda, Kivule, Mzinga na Kipunguni ikiwa ni utaratibu wake wa kuwafikia wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
Katika ziara hiyo Mhe. Mpogolo aliambatana na Wataalam kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na wengine kutoka Taasisi wezeshi zinazowahudumia wananchi kwa ukaribu zaidi pamoja na timu ya Wanasheria kutoka Wilayani.
Akiwa katika kusikiliza kero za wananchi wa Kata hizo, Mhe. Mpogolo amesema amebaini kero kubwa kutoka kwa wananchi wa Kata hizo zikiwemo Barabara zisizopitika, ukosefu wa Soko na uvamizi wa ardhi.
Hata hivyo, Mhe. Mpogolo amewataka Viongozi wa Serikali za Mitaa kuhakikisha wanasimamia vizuri suala la ardhi hususani maeneo yaliyoachwa wazi kwani maeneo hayo ya naweza kutumia kuendeleza miundombinu ya Afya, Elimu na Barabara.
“Niwaombe Viongozi wa Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na wataalamu wetu kuhakikisha mnasimamia vizuri Ardhi isivamiwe kwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Elimu, Afya na Barabara hivyo maeneo hayo yatasaidia katika utekelezaji wa miradi hiyo ya Maendeleo hivyo muhakikishe mnatunza ardhi na mkiuza viwanja au kujenga muhakikishe mnaacha njia za kupita barabara.”
Kwa upande mwingine, Mhe. Mpogolo amewasihi wanawake hususani mama lishe kuachana na mikopo yenye riba kubwa badala yake waunde vikundi ili waweze kukopa mikopo ya asilimia 10% ya Halmashauri kwani mikopo hiyo ya Wanawake, vijana na watu wa Makundi maalumu haina riba.
Halikadhalika, Mhe. Mpogolo amewataka Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari kutumia utaratibu maalumu wa kufanya mitihani wananfunzi na sio kila mara kudai ada za mitihani kwani wana waumiza wazazi wenye kipato cha chini huku akiwasisitiza wazazi kuwa wanafunzi kula chakula ni muhimu hivyo wahakikishe wanachangia ada ya chakula.
Post A Comment: