Mkuu wa Wilaya ya Ilala  Mhe. Edward Mpogolo amewataka Viongozi wa Matawi, Mashina, Mitaa na Kata  Kutimiza Majukumu yao kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 sambamba na Kauli mbiu isemayo “Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”.

Mhe. Mpogolo ametoa wito huo Septemba 13, 2024 wakati akifanya Semina na viongozi hao katika Ukumbi wa Wikicha uliopo Banana - Jijini Dar es Salaam iliyolenga kuwakumbusha majukumu yao ya kuwahamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la Makazi ili waweze kushiriki kupiga kura.

Nipende kuwashukuru sana kwa kujitokeza kwa wingi kwenye Semina hii ambayo ni chachu ya maendeleo katika Jiji letu na Taifa kwa ujumla , hivyo nichukue nafasi hii kuwahimiza mhakikishe mnajiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura katika makazi yenu mnayoishi  pamoja na kuhakikisha mnawahamasisha wananchi kujiandikisha ili waweze kupiga kura kuchagua viongozi bora na wanaowapenda kwa maendeleo ya Kata zetu, Wilaya na Taifa kwa ujumla  kwani ili uweze kupiga kura nilazima uwe umejiandikisha kwenye daftari katika Mtaa wako  husika ambao umekua unaishi hivyo nitoe wito kwenu kuhakikisha mnawakumbusha wananchi kujiandikisha pamoja na kuhakikisha mnajua sifa zote za mpiga kura ili pindi zoezi likifunguliwa tarehe 11 Octoba, 2024 wananchi hao wawe wanajua ni sifa zipi anatakiwa kuwa nazo ili ajiandikishe”. Amesisitiza Mhe.Mpogolo.

Katika hatua nyingine, Mhe.Mpogolo ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa sana katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kwani zaidi ya Billion 100 zimepokelewa na Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Afya na Miundombinu ya barabara ambapo miradi hii ni chachu ya kuboresha huduma za jamii kwa wananchi na kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma bora na kwa wakati.

Share To:

Post A Comment: