Na Munir Shemweta, WANMM

Changamoto ya usafiri inayowakabili watumishi wa wizara ya ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi sasa inaenda kupungua kufuatia wizara hiyo kukabidhiwa basi jipya aina ya TATA lenye thamani ya shilingi milioni 170.

Makabidhiano ya gari hiyo yamefanyika jijini Dodoma leo Septemba 19, 2024 baina ya Meneja Uendeshaji wa Kampuni ya TATA Africa Holdings (Tanzania) Limited Bi. Muareen Kiputa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Seushi Mbuli kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo na kuhudhuriwa na baadhi ya watumishi wa wizara Makao Makuu.

Kupatikana kwa basi hilo kuinaifanya Wizara ya Ardhi kuwa na mabasi matatu yatakayopunguza changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hususan pale wanapokwenda na kurudi ofisini sambamba na shughuli nyingine za wizara nje ya makao makuu ya wizara.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Ardhi Bw. Seushi Mbuli amesema, kupatikana kwa basi hilo kutapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya usafiri kwa watumishi wa wizara hiyo hasa pale wanapokweda na kurudi maofisini.

Ameongeza kuwa, kununuliwa kwa basi hilo ni jitihada za Wizara ya Ardhi kuhakikisha watumishi wake hawapati shida ya usafiri wakati wa kwenda kutekeleza majukumu yao katika maeneo mbalimbali.

‘’Nina imani kubwa sasa changamoto ya usafiri kwa watumishi wetu itapungua sana kutokana na ujio wa basi hili’’. alisema Mbuli



Share To:

Post A Comment: