Na, Elizabeth Paulo; Dodoma 

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chemba limelaani vikali kitendo kilichotokea hivi karibuni la Mganga wa Kienyeji aliyetuhumiwa kwa mauaji mkoani Singida na mji mwingine Wilayani Chemba, Mkoa wa Dodoma ambako yamebainika mashimo sita walimozikwa watu.

Akizungumza Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Chemba Saidi Sambala katika kikao cha Baraza la Madiwani amesema wanalipongeza jeshi la polisi kwa kufanya upelelezi na kubaini jumla ya miili ya watu 10 waliouawa.

Katika Taarifa iliyotolewa Agosti 26,2024 na msemaji wa Jeshi la polisi, David Misime imesema katika mwendelezo wa uchunguzi wamebaini miili ya watu 10  waliouawa kati ya hiyo mitatu ilipatikana Mkoani Singida na Dodoma ilipatikana saba .

Kati ya Miili hiyo, Amesema mmoja ulitupwa porini na mingine tisa ilizikwa kwa kukalishwa kwenye shimo kwa namna wahisika walivyosukumwa na imani zao  za kishirikina.

Aidha Jeshi la polisi linatoa woto kwa Wananc0hi kuendelea kutoa taarifa za kweli na Sahihi na kuendelea kukemea kuanzia ngazi ya familia ili kuzuia na kukomesha vitendom vinavyoendelea kutokea ndani ya Jamii kwa Siri kubwa .

Wakizungumza  mara baada ya kikao cha Baraza baadhi ya Madiwani wameiomba Jeshi la Polisi  kuendelea kuisaidia jamii kwa kuendeleza uchunguzi wa matukio mbalimbali kama yalivyotokea Dodoma na Singida ili kubaini watu wengine wanaotekeleza uhalifu.

Aidha wamesema hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wahusika ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Share To:

Post A Comment: