Kampuni ya simu za mkononi Airtel kupitia kwa Mkurugenzi wa Biashara Joseph Muhele amesema kuwa mtandao huo mwaka huu 2024 unaendelea kufangua huduma zake za mawasiliano katika miji na Vijiji ambapo kwa mjini kuwezesha kupata huduma ya 3G,4G,5G na Kampuni inaendelea na Uwekezaji na upanuzi wa mtandao maeneo ya Vijiji ili kuwezesha kupata huduma ya 3G 4G na 5G.
Aidha ameeleza kuwa kwa mwaka 2013 kampuni hiyo ilifunga mtambo mpya Submarinecable ambao ni mkubwa wenye uwezo wa kupokea na kutumia data kwa kiwango kikubwa ,uwekezaji huo umefanywa kwa ajili ya Watanzania na nchi jirani kwajili ya mawasiliano.
Muhele ameendelea kufafanua kuwa lengo la Mkutano huo wa 8 ni kuwaleta Wadau wote pamoja katika teknolojia, ambapo kampuni hiyo inaendelea kuvifikia Vijiji vyote ambavyo havijafikiwa na huduma hiyo ambapo sasa wanajenga huduma ya 5G kwa ajili ya wateja Ujenzi ambao unaenda sambamba na kuhakikisha gharama zinakuwa nafuu.
Kwa upande wake Waziri wa Habari ,Mawasiliano Teknolojia ya habari Jerry Slaa akifungua kogamano hilo la siku mbili (Connect2Connect Summit) ambapo limewakutanisha wadau wote wa Mawasiliano nchini pamoja na wadau wengine ambapo amesema Watanzania zaidi ya Mil.75 wana simu za mkononi 35% wanamtandao wa intaneti ambapo mwaka mei 2023 Serikali ilizindua mkakati wa ujenzi wa minara 758 kupitia USAF mfuko uliotengenezwa na seeikali ambapo kila mtoa huduma anachangia ili kupeleke huduma
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo Mhe. Always alisema minara mingine 636 mradi huo utaanza Oktoba 2024 huku akiwatak wananchi wanaofanya shughuli zao kupitia mitandao wapo salama zaidi na Serikali imetunga Sheria ya kulinda data za mtu binafsi katika matumizi ya mtandao na kila mtumiaji analindwa na hairuhusiwi kutumia data za mtu bila ridhaa yake.
Aidha Waziri Slaa,amesema hadi sasa 89% ya Watanzania wanapata huduma mtandao lengo likiwa Wananchi wote wapate huduma ya mtandao wa Internet,simu ,habari ,redio na televisioni yakuwemo maeneo ya Utalii ambayo yamepewa kipaumbele
Kwa upande wake injinia Cecil Mkomola Francis mkurugenzi wa ufundi na Uendeshaji wa Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL amesema wanadhamana kubwa ya kutoa huduma ya mawasiliano, kupitia mkongo wa mawasiliano wa Taifa kwani wameendelea kufanya kazi na kuhakikisha kuwa nchi inaongea kwa kuunganishwa mikoa wilaya ambapo jumla ya wilaya 106 zimeunganishwa Tanzanzania bara Kati ya wilaya 139,mkongo huo ndio kiungo kikuu cha Mawasiliano na Intaneti.
Amesema kuwa kazi kubwa waliyonayo kama Shirika ni kutoa mchango mkubwa wa mawasiliano kuhakikisha kwamba wanafikisha huduma kwa Wananchi na kupungiza gharama za matumizi
upande wake ,Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la mhandis Francis Mkomola,amesema Shirika hilo lina dhamana kubwa ya kutoa huduma bora za mawasiliano kupitia mkongo wa taifa ambao ulianza kutekeleza mwaka 2013.
Vilevile wameunda mkongo huo na nchi jirani za Kenya,Uganda ,Rwanda,Burundi ,Zambia,Malawi na kuna maunganusho yanayoenda kwenye mpaka na Msumbijina sasa wanaanza kushughulikia maunganusho na nchi ya DRC Congo,kupitia ziwa Tanganyika hadi mji wa Kalemii Nchini DRC pia wanashugulikia maunganisho kwenda kwenye kituo kilichopo baharini hadi Mombasa Nchini Kenya.
TTCL inaendelea kutoa mchango wa mawasiliano kuhakikisha mkongo unaojengwa inakuwa na ubora wa hali ya juu kwa lengo la kufikisha huduma kwa Wananchi na kupunguza gharama ambapo Tanzania ni kiunganishi kikuu cha Mawasiliano kwenye ukanda wa nchi za EAC na SADC, wilaya ambazo hazijaunganishwa kwenye mkongo wa taifa zitaunganishwa mwaka huu na wakandarasi wapo wanaendelea na shughuli hiyo
Mkutano huu umehusisha wadau wote wa mawasiliano nchini Tanzania chini ya kauli mbiu ya ‘Meaningful Connectivity’
Post A Comment: