Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika akiongea na wananchi wa kanda ya kusini wakati wa maonyesho ya nane nane ya 31 mkoani Lindi
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika akichukua juice ya iliyotengenezwa kwa zao la Korosho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika akifurahia jambo la kijana anaye kunywa juisi ya korosho
Na Fredy Mgunda, Lindi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mh. George Mkuchika amewataka watanzania kula korosho pamoja na bidhaa zingine ambazo zinatokana na zao la korosho kwa kuwa zina faida kubwa sana kwa binadamu.
Akizungumza leo kwenye maoyesho ya wakulima maarufu kama Nane nane Kanda ya Kusini yanayoendelea katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi, Waziri huyo amesema korosho ni lishe na kwamba zina viini lishe vya kutia joto na protin mara mbili zaidi kuliko nyama na samaki.
Korosho zina madini muhimu mwilini kama sodium , copper, potassium, magnesium, phosphorus, chuma na zink madini.
"Madini haya ni muhimu kwa ajili ya kuilinda miili yetu pamoja na mishipa ya fahamu," amesema.
Amesema ulaji wa korosho una faida ya kuzuia ugonjwa wa moyo, kuongeza chembechembe hai nyekundu, nakuongeza viini lishe vinavyozuia hatari ya kupata ugonjwa wa kansa.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuchika amewataka vijana na wanawake kujihusisha katika shughuli ya uongezaji wa thamani wa zao la korosho ili kutanua wigo wa matumizi ya Korosho na bidhaa zake.
Post A Comment: