Na Bulugu  Magege.

KUNA muda unafika Vijana wanapaswa kusimama imara, kuchukua hatua, na kuwa sehemu ya historia bora inayoandikwa katika nchi na taifa analoishi.

Nchi ya Tanzania inapoelekea katika uchaguzi wa Serikali ya Mitaa mwaka huu na uchaguzi Mkuu mwaka 2025,sauti ya kijana ni muhimu zaidi kuliko wakati wowote ule.

Kijana ni mtu ambaye anaweza kuwa na nguvu ya kuleta mabadiliko na kubadili mwelekeo mzuri wa taifa zima kutokana na sauti yake.

Kura moja ya kijana wa Kitanzania,inamaana kubwa ya kuleta mabadiliko katika nchi na jamii kwani kura ni tone la maji katika bahari kubwa ya demokrasia.

Ni jambo jema kwa vijana kuchagua kiongozi bora,kujitokeza kugombea nafasi za uongozi na kujiandikisha katika daftari la kupiga kura  na kupata nafasi ya kuandika mustakabali wako mwenyewe na mustakabali bora wa taifa letu.

Kwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi,kijana anaweka alama yake katika historia ya taifa la Tanzania, alama itakayokumbukwa na vizazi vijavyo hususan katika dunia ambayo inakabiliwa na changamoto za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

Ushiriki wa kijana ni muhimu katika kujenga jamii ya kitanzania inayozingatia haki, usawa na maendeleo ya taifa la Tanzania.

Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan aliwahi kusema"Youth participation in decision-making is not only a right but also a necessity if we want a more democratic, inclusive, and sustainable future."(Katika hotuba ya International Youth Conference,July 2006).

Maneno haya yanamaana kuwa Ushiriki wa vijana katika maamuzi si haki tu bali ni hitaji muhimu kwa ajili ya kujenga jamii inayoheshimu Demokrasia, Ushirikishwaji na Maendeleo endelevu.

Hii ina maana kwamba  bila ushiriki wa vijana,mipango ya Maendeleo inaweza kukosa mtazamo wa kizazi chetu(Vijana), ambao una ndoto na mawazo mapya ya kuendeleza taifa.

Vijana wanaposhiriki kikamilifu,wanachangia katika kuunda sera bora ambazo zinazingatia mahitaji na matarajio yao na Jamii kwa ujumla.

Naye,Ban Ki-moon,aliyewahikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, aliwahi kusema "Young people are the leaders of tomorrow, but they are also the leaders of today. Their voices matter in shaping the policies and decisions that will impact their futures."(Remarks at the Global Youth Forum, December 2012)

Maneno haya yana maana kuwa "Vijana ni viongozi wa kesho, wao pia ni viongozi wa leo.Sauti zao ni muhimu katika kuunda sera na maamuzi ambayo yataathiri mustakabali wao."

Ni muhimu kwetu vijana wa Kitanzania,kuwa na ushiriki wa moja kwa moja katika mchakato wa uchaguzi na uongozi ,Mwezi Novemba 2024 Tanzania itakuwa na uchaguzi wa serikali za mitaa hivyo wakati ni wetu vijana sasa kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbali mbali kwa namna zitavyotangazwa na Tume huru ya Uchaguzi(NEC).

Mbali na kujitokeza kugombea pia Vijana wanatakiwa  kushiriki kikamilifu kwa kuchagua viongozi bora,wazalendo na wanaoweka maslai ya jamii na maslai ya taifa mbele.Vijana tunajukumu la kujenga Tanzania bora ya leo na kesho

Agosti 6,2024 Rais Dkt Samia Suluhu Hassan,akiwa Mkoani Morogoro kwenye ziara ya kikazi,Rais Samia aliwaambia vijana na UVCCM "Kazimeni zote, kawasheni kijani."

Hapa Rais Dkt Samia alimaanisha kuwa vijana wanapaswa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa uchaguzi 2024-2025  kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia ushiriki wao, kama vile kutojiandikisha au kutokujitokeza kupiga kura na Kugombea.

''Kazimeni zote''Pia anawakumbusha vijana kuwa nguvu ya kushinda vikwazo na kufanya kila iwezavyo ili kuhakikisha wanajiandikisha katika daftari la wapiga kura, kupiga kura,  kuchagua viongozi bora na Kugombea.

"Kawasheni kijani" Anasisitiza kuwa vijana wanapaswa kutumia nguvu zao na Umoja wao kuleta mabadiliko chanya, kwa kuchagua viongozi wenye maono na uongozi bora, na hata kugombea nafasi za uongozi wao wenyewe.

Rais Dkt Samia hakuishia hapa aliwataka vijana wawe na sauti kubwa katika kuunda mwelekeo wa taifa lao, kuhakikisha kuwa maamuzi yanayofanywa ni ya haki na yanazingatia matarajio yao na ya taifa kiujumla.

Kampeni hiyo kubwa ya Tunazima Zote, Tunawa Kijani" iliyozinduliwa na UVCCM chini ya Mwenyekiti,Mohammed Ally Kawaida,Makamu Mwenyekiti wa UVCCM,Rehema Sombi na Katibu Mkuu Jokate Mwegelo,mnamo Julai 6,2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar-es-Salaam, na pia  Zanzibar Agosti 10,2024, ni juhudi za Viongozi wa UVCCM,jumuiya pekee yenye dhamana na Vijana kuhamasisha vijana kushiriki kikamilifu katika mchakato huu.

Lengo kuu la kampeni hiyo ni kuamsha hamasa ya Vijana  kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, kujitokeza kupiga kura, kuchagua viongozi bora, na hata kugombea nafasi za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 2024 na uchaguzi mkuu ujao 2025.

Ushiriki wa vijana kikamilifu una faida nyingi kwa taifa letu ikiwemo Kuimarisha Demokrasia,Kuchagua Viongozi Bora,Kuleta Mabadiliko bora ya Kudumu na kufanya

Vijana wanapogombea nafasi za uongozi mbali mbali, wanapata nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika kuleta mabadiliko chanya  ya kijamii na kiuchumi katika taifa letu.

Katika kitabu chake "Why We Vote: How Schools and Communities Shape Our Civic Life" (2014) ,Mwandishi Dana.R.Fisher,  kwa muhtasari, Dana R. Fisher ni profesa wa Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Maryland, College Park, Marekani. katika kitabu chake hicho anawashauri Vijana kushiriki kikamilifu katika uchuguzi ili kujenga jamii bora

 

Mfano katika ukurasa wa 145 ana sema "Young people’s involvement in voting not only helps them to develop their own political identity but also strengthens the democratic process by ensuring that diverse perspectives are represented in our political system."

Kwa kiswahili akimaanisha "Ushiriki wa vijana katika kupiga kura hauwasaidii tu kuunda utambulisho wao wa kisiasa, bali pia unaimarisha mchakato wa kidemokrasia kwa kuhakikisha kwamba mitazamo mbalimbali inawakilishwa katika mfumo wetu wa kisiasa."

Rais  wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema haki, demokrasia, sheria na utawala bora utadumishwa kwa Watu wote wakati wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Rais Samia Dkt Samia  aliwahisema  katika sherehe za mwaka mpya 2024 (Diplomatic Sherry Party) kuwa uchaguzi huu utakuwa huru, amani na wa haki na mara kwa mara amekuwa akisema, hivyo vijana tutumize haki yetu kwa kukishiriki kikamilifu.

Pia Rais Dkt samia, August 06,2024 wakati akihutubia mkutano wa hadhara uwanja wa Jamhuri Mkoani Morogoro, Rais Samia alisema

“Ifikapo November mwaka huu tuna kijambo chetu si ndio?, Chaguzi za Serikali za Mitaa, niwaombe kawekeni Viongozi wapenda maendeleo watakaowafanyia kazi Wananchi kwenye maendeleo ili ile fedha itakapokuwa inashuka kuja kuondosha changamoto za Wananchi, kuwe na Viongozi mahiri kule chini wa kusimamia na kuhakikisha inatumika vizuri na Viongozi hawa wanatoka Chama gani!?”

Vijana tunajukumu la kumuunga mkono Rais wetu Dkt Samia kwa kuchagua Viongozi bora, Viongozi wazalendo, wanaoweka maslahi ya taifa mbele, Viongozi waadilifu na wenye maono.

 

Bulugu  Magege

0655-248822

Bulugu.magege22@gmail.com

 

 

 

 

000000000000000000000000000

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: