Na Okuly Julius Dodoma
Mbunge wa viti maalum kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye pia ni muwakilishi wa wanawake mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagende amelipongeza shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL kwa kuifungia nchi katika eneo la Mawasiliano.
Amesema maboresho makubwa yaliyoyafanywa na TTCL katika kuhudumia umma wa watanzania hasa katika ulimwengu wa kidigitali hakuna yeyote anayeweza kutia shaka katika hilo .
Akizungumza leo Agosti 06,2024 Jijini Dodoma mara baada ya kutembelea banda la Shirika hilo lililopo kwenye maonesho ya Nanenane Nzuguni, Mwakagenda amesema Shirika hilo limefanya maboresho makubwa kuendana na wakati uliopo sasa kwani wanawafikishia huduma wananchi mpaka kwenye makazi yao kwa kupitia huduma yao ya fiber Mlangoni.
“Niipongeze sana Serikali chini ya usimamizi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kupitia shirika hili la TCCL kwa uwekezaji mkubwa uliofanyika tumeona sasa mtandao wa interneti unapatikana kila sehemu na ukizingatia sasa hivi Dunia ipo kiganjani”,Amesema.
Amesema maboresho yaliyoafanyika wao kama jicho la pili la serikali wameridhishwa na kuahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha mtandao wa TTCL unafika mbali zaidi.
Ameongeza kuwa ufanyaji wa biashara kwa sasa unategemea zaidi mtandao lakini pia kuanza kwa treni ya umeme SGR kunategemea zaidi mtandao haswa katika ukataji wa treni ili kupunguza msululu kwenye madirisha ya kukatia tiketi.
Sambamba na hayo Mwakagenda ametoa rai kwa shirika hilo kuhakikisha wanafikisha huduma ya intaneti kwa shule za sekondari zilizopo vjijini ili kuwasaidia kujifunza.
“Niwaombe TTCL kupeleka huduma hii kwa shule za sekondari zilizopo vijijini wapate huduma hii kwenye maktaba zao na maabara zao ili waweze kujifunza kwa vitendo”,Ameongeza Kagenda.
Kwa upande wake Meneja Biashara TTCL Dodoma Leyla Pongwe amesema TTCL kupitia kampuni Tanzu T-PESA imekuja na huduma ya MALIPO KWA MKUPUA inayowezesha Shirika, Taasisi au Kampuni kuweza kuwalipa wanufaika wake kwa haraka.
Amesema huduma hiyo inawasaidia wakulima kupitia vyama vyao vya ushirika ambapo Chama cha ushirika kinaweza kuwalipa wakulima na wakapokea fedha kupitia simu zao za Mkononi kwa wakati mmoja.
"uzuri wa huduma hii ni kwamba Mkulima anaweza kupokea ujumbe wa Malipo kupitia laini yeyote sio lazima awe na laini ya TTCL hapana," ameeleza Bi. Leyla
Amesema kupitia maonesho ya Kimataifa ya Nanenane TTCL inajivunia kufikisha huduma ya Mawasilino juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro ambapo sasa watalii hawana tena Shida ya internet wanapotembelea mlima huo.
Post A Comment: