Na Mapuli Kitina Misalaba

Taasisi ya Wanawake na Samia Shinyanga imefanya tukio la kupanda miti na kutoa msaada wa taulo na sabuni katika Kituo cha Afya Kambarage, Shule ya Msingi Ibadakuli, na Shule ya (Shinyanga Girls) Wasichana Butengwa, zote zikiwa katika Manispaa ya Shinyanga.

Katika Kituo cha Afya Kambarage, taasisi hiyo imetoa msaada wa sabuni kwenye wodi ya wazazi, na katika Shule ya Msingi Ibadakuli na Shule ya Wasichana Butengwa, wamegawa taulo kwa wanafunzi wa kike.

 Aidha, wamepanda miti katika maeneo hayo ili kuboresha mazingira na kuongeza uhamasishaji juu ya umuhimu wa usafi wa mwili na mazingira.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa Shinyanga, Husna Mashaka Ally, amesema zaidi ya miti mia moja imepandwa na taasisi hiyo.

 Viongozi wengine wa Taasisi ya Wanawake na Samia Shinyanga wamesisitiza umuhimu wa usafi wa mwili na mazingira, hususan kwa wanafunzi, ili kujenga afya bora na mazingira safi kwa wote.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage Dkt. Ernest Magula pamoja na walimu wa shule zilizopokea msaada, wameishukuru na kuipongeza taasisi hiyo kwa mchango wao mkubwa wa kupanda miti na kutoa msaada kwa wanawake na wasichana.

Baadhi ya wanawake waliopokea msaada wa sabuni katika Kituo cha Afya Kambarage na wanafunzi katika shule hizo nao wameishukuru taasisi hiyo kwa msaada waliopewa.

 

Tukio hili linaonyesha jitihada za Taasisi ya Wanawake na Samia Shinyanga katika kuboresha mazingira na afya za wakazi wa Shinyanga, hususan wanawake na wasichana.

 Picha ya pamoja katika eneo la kituo cha Afya Kambarage mjini Shinyanga leo Agosti 2,2024.

 

Share To:

Misalaba

Post A Comment: