Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). Mhe. Ridiwani Jakaya Kikwete amesema serikali ipotayari kuendelea kuwasikiliza vijana juu ya mahitaji ya na kuyafanyia kazi kwa wakati.

Mhe. Kikwete ameyasema hayo Julai 31, 2024 katika Kongamano la Vijana lililoandaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali ya DOYODO kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Kikwete pia ametumia Jukwaa hilo kuwaeleza vijana juu ya nia ya serikali kuendelea kuwahudumia vijana katika maeneo mbalimbali ya kimaisha na utayari wa serikali kukutana nao huko kwenye ngazi za chini za maamuzi ili kwa pamoja kukabili changamoto walizonazo.

"Katika kupitia programu mbalimbali zinazoendeshwa pamoja na marekebisho na sera na sheria ili ziendane na mahitaji ya vijana hapa nchini ninawahakikishia serikali itakutana na vijana katika kila ngazi ili kuweza kuwasikiliza na kuhakikisha inawagusa katika hali ya kunuana kiuchumi ili kuwa na Taifa bora lenye nguvu kazi na uchumi imara". Amesema Kikwete.


Aidha pamoja na hayo Mhe. Kikwete amewaahidi vijana kuwa serikali yao itawasikiliza na kuyafanyia kazi mahitaji yao ikiwemo la ajira na mitaji kuwawezesha kufanya biashara na shughuli nyengine za kipato.



Share To:

Post A Comment: