Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Selemani Jafo(Mb) amebainisha hatua ambazo Serikali inazichukua katika kuhakikisha inaendelea kusimamia ushindani wa haki na kuwalinda watumiaji wa bidhaa na huduma hapa nchini, kwa kutumia Sheria ya Ushindani Na.8 ya Mwaka 2003 ambayo inatarajiwa kufanyiwa marekebisho katika mkutano huu wa Bunge kwa lengo la kuongeza tija katika kumlinda mlaji.

Mhe.Jafo ameeleza mikakati hiyo bungeni jijini Dodoma wakati wa kujibu swali la Mbunge wa Muleba Kusini, Mhe.Dkt.Oscar Ishengoma Kikoyo.

Katika swali lake, Mhe. Kikoyo alitaka kujuwa, lini Serikali itatenganisha dhana ya ushindani na dhana ya kuwalinda watumiaji wa bidhaa na huduma nchini.

Akijibu swali hilo, Mhe. Jafo amesema, kimsingi dhana ya ushindani na kumlinda mlaji zina uhusiano mkubwa kwasababu ushindani wenye afya katika soko ni mojawapo ya njia bora ya kumlinda mlaji.

Aidha,ameongeza kuwa kupitia ushindani, mteja ananufaika kwa kupata unafuu wa bei, kuongezeka kwa wigo wa kupata bidhaa bora na chaguo sahihi la mlaji, kukuza ubunifu wa wazalishaji wa bidhaa na kudhibiti ukiritimba katika soko.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: