Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kukuza sekta za uzalishaji  ikiwemo Kilimo, Mifugo na uvuvi kwa lengo la kuzalisha kwa tija na kuongeza fursa za ajira katika sekta hiyo.

Amesema katika kutekeleza hilo, Serikali imeongeza bajeti ya sekta hiyo ambapo Wizara ya Kilimo bajeti imeongezeka kutoka Bilioni 294 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi Trilioni 1.3 mwaka wa fedha 2024/2025.

Mhe. Ridhiwani amesema hayo leo Agosti 8, 2024 Jijini Mbeya katika Viwanja vya John Mwakangale wakati wa kilele cha Maonesho na sherehe za Wakulima (Nanenane) kanda ya Nyanda za juu kusini.

Awali akizungumza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnnyeti amesema Wizara ya Mifugo kwa kushirikiana na sekta binafsi inaendelea kutekeleza programu ya mafunzo atamizi ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji kwa vijana ili waweze kujiajiri.







Share To:

Post A Comment: