Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akifungua mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoani Shinyanga leo Agosti 28,2024.
Na Mapuli Kitina Misalaba
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ametoa wito kwa mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria za nchi na kuheshimu utamaduni wa Kitanzania.
Akizungumza kama mgeni rasmi leo, Agosti 28, 2024, wakati wa kufungua mkutano wa jukwaa la mashirika hayo mkoani Shinyanga, RC Macha amesisitiza umuhimu wa kufuata sheria ili kuhakikisha ushirikiano wa karibu na serikali unadumishwa.
"Serikali inatambua na kuthamini mchango wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika maendeleo ya jamii, na tutaendelea kushirikiana nanyi hata hivyo, ni muhimu kuhakikisha kwamba mnatekeleza wajibu wenu kwa kuzingatia sheria na utamaduni wa nchi yetu," amesema Macha.
Aidha, amewapongeza viongozi wa mashirika hayo kwa kuajiri vijana na kuchangia kupunguza tatizo la ajira nchini huku akisisitiza umuhimu wa ajira hizo kutolewa kwa haki na kuzingatia vigezo vya kitaaluma badala ya upendeleo wa kifamilia.
Pia, RC Macha ameonya mashirika hayo kutokuingilia mamlaka za utawala za maeneo wanayofanyia kazi, na badala yake, kuhakikisha wanashirikiana na viongozi wa maeneo husika ili kufanikisha utekelezaji wa miradi yao kwa ufanisi zaidi.
Akisoma risala ya mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali, Mwenyekiti wa NGO’s Mkoa wa Shinyanga, Bwana Bakari Juma Kibile, alitoa shukrani kwa serikali ya mkoa na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya mashirika yasiyo ya kiserikali na serikali katika kuleta maendeleo endelevu.
Kibile amebainisha kuwa mashirika 116 yaliyosajiliwa mkoani humo yanaendelea kutoa huduma muhimu kwa jamii, ikiwemo elimu, afya, haki za binadamu, na ujasiriamali.
Vilevile, ameeleza kuwa mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kupambana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake, huku akiomba serikali kuendelea kuboresha mazingira ya utekelezaji wa miradi yao kwa kutoa vibali kwa wakati na kuhamasisha mahusiano mazuri kati ya serikali na mashirika hayo.
Washiriki wa mkutano huo wameishukuru serikali kwa ushirikiano wanaoupata na kuomba kuwepo kwa miradi ya ndani ili kupunguza utegemezi wa miradi inayofadhiliwa kutoka nje ya nchi.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga ambapo RC Macha ameahidi kuendelea kuwa mlezi wa mashirika hayo na kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya mkoa wa Shinyanga.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akizungumza kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.
Mwenyekiti wa NGO’s Mkoa wa Shinyanga, Bwana Bakari Juma Kibile, akisoma risala ya mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha leo Agosti 28,2024.
Mwenyekiti wa NGO’s Mkoa wa Shinyanga, Bwana Bakari Juma Kibile, akisoma risala ya mashirika hayo yasiyokuwa ya kiserikali kwa Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha leo Agosti 28,2024.
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akisoma maazimio kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga Bi. Rehema Edson akisoma maazimio kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga, Bestina Gunje akisoma mapendekezo ya kamati ya ushauri wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.
Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga, Bestina Gunje akisoma mapendekezo ya kamati ya ushauri wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga, Bestina Gunje akisoma mapendekezo ya kamati ya ushauri wa mashirika yasiyo ya kiserikali, kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga leo Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Women and Youth Development Solution (WAYDS Tanzania) Bwana Charles Deogratius akitoa maoni yake kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.Afisa program wa shirika la WELDAF, Bi. Joyce Kessy akitoa maoni yake kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.
Mkurugenzi wa shirika la Lifeline Cocenselly Centre and gender empowerment Dkt. Meshack Kulwa akitoa maoni yake kwenye mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.
Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.
Mkutano wa jukwaa la mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) mkoa wa Shinyanga ukiendelea katika ukumbi wa mikutano ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Agosti 28,2024.
Post A Comment: