Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Mhandisi Juma Hamsini amemkabidhi ofisi Mkurugenzi mpya wa Jiji la Arusha Bwana John Kayombo.
Makabidhiano hayo yameshuhudiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mhe. Felician Mtahengerwa, Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, kamati fedha na wataalamu kutoka Halmashauri ya Jiji la Arusha.
Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amesema, Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ipo tayari kutoa ushirikiano kwa Mkurugenzi Kayombo hasa katika kusukuma miradi ya maendeleo.
Aidha, amesisitiza kufanya kazi kwa ushirikiano baini ya viongozi na wataalamu ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Jiji la Arusha.
Naye, Mkurugenzi Kayombo amesema yeye kipaombele chake ni ukusanyaji wa mapato kwa asilimia mia Moja na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo.
Amesema ili kufanikisha hilo, ushirikiano baina ya viongozi wote na wataalamu ndio njia sahihi na kufanya kazi kwa bidii nakwa ubunifu.
Kwa upande wake Mhandisi Juma Hamsini, amelishukuru Baraza la Madiwani na watumishi wote kwa ushirikiano waliouonesha kwake na kuomba uendelee hata kwa Mkurugenzi Kayombo.
Kwa Upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqe amesema yeye na Baraza lake wapo tayari kushirikiana na Mkurugenzi Kayombo katika ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa wakati.
Makabidhiano ya ofisi kwa wakurugenzi hao yametokana na mabadiliko ya uteuzi yaliyofanywa mnamo Agosti 14,2024 na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Sami Suluhu Hassan, kwa Mhandisi Juma Hamsini kuhamishiwa Jiji la Tanga na bwana John Kayombo kupangiwa Halmashauri ya Jiji la Arusha akitokea Jiji la Dodoma.
Post A Comment: