Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MKURUGENZI wa Idara ya Usalama na Mazingira Wizara ya Ujenzi Mhandisi Kashinde Musa, amesema katika jitihada za kulinda barabara nchini ambazo serikali imewekeza fedha nyingi wamefunga mizani 78 nchini kwa ajili ya kudhibiti uzito wa magari.

Mhandisi Musa, amesema hayo leo Agosti 27,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushiriki wao kwenye wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani inayofanyika kitaifa jijini hapa.

Amesema, serikali iimewekeza fedha nyingi katika ujenzi wa miundombinu ya barabara lakini moja kati ya chanamoto ni uharibifu kutokana na magari kubeba mizigo mizoto Zaidi ya uwezo wa barabra.

“Niwatake wadau wote wa usafirishaji nchini kuhakikisha kuwa wanafuta taratibu na kanuni za uziti barabarani ili barabara zetu ziweze kudumu kwa mijibu wa muda ule ambao umekusudiwa”amesema

Aidha, amesema ili kupunguza ongezeko la ajali nchini wizara hiyo katika mwaka huu wa fedha imetenga bajeti kwa ajili ya kupunguza msongamano wa magari katika majiji matano.

Ameyataja majiji hayo kuwa ni Arusha, Dodoma, Mwanza, Mbeya na Dar es Saalam.

“Mradi huu utakapo kamilika tunatarajia utasaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo lakini lengo letu ni kuhahakikisha maradi huu unakwenda nchi nzima”amesema

Amesema pia wizara imejikita katika matumizi ya teknolijia sa kisasa kwa ajili ya kupunguza ajali katika maeneo mbalimbali ikiwemo ufungaji wa camera za usalama.

“Kuna mradi wa majaribu wa ufugaji wa kamera ambao tuliufanya katika mikoa ya Pwani na Morogo mwaka 2016 ambao tumebaini kuwa tangu wakati huo tulipofunga kamaera hizo ajali zimepungua kwa kiasi kikubwa sana hivyo lengo letu ni kufunga kamera hizo nchi nzima”amesema

Aidha, amesema moja ya changamoto ambayo inawakabili hivi sasa ni uharibifu na wizi wa alama za usalama barabarani ambazo kwa namna moja imekuwa ikisababisha ajali.

“Changamoto tunaweka alama za barabarani lakini wizi wa alama hizo ni tatizo lakini tumekuwa tukitoa elimu kwa wanahi kuacha kufanya hivyo lakini pia wanaobainika hatua za kisheria zinachukuliwa dhidi yao”amesema

Meneja wa Mazingira na Jamii Wakala wa Barabara nchini Tanroad, Zafarani Madayi, alisema kila mtu anao wajibu wa kutunza miundombinu ya barabara.

Amesema, wananchi wanapaswa kutunza miundombinu ya baraba na kuacha kufanya shughuli zozote za kibinadamu kwenye hifadhi ya barabara.

“Sheria inakataza watu kufanya shughuli yoyote ya kibinadamu katika hifadhi ya barabara na kwa mujibu wa sheria eneo la hifadhi ya barabara ni mita 60 yaani mita 30 kila upande”amesema

Kadhalika, amewataka wanachi kuacha kuchoma moto moti na majani kwenye barabara pamoja na kupitisha mifugo ili kuepusha kingo za barabara kumegeka.






Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: