Meya wa Jiji la Arusha Maximillan Iraghe akishiriki Mbio za Clock Tower Marathon na kukimbia mbio hizo kilomita 10 zilianzia na kuishia kwenye uwanja wa Gymkana Jijini Arusha.
Meya wa Jiji la Arusha Maximillan Iraghe amewataka waratibu wa mbio za Clock Tower kuzifanya mbio hizo kuwa za kipekee zinazokimbiwa ndani ya Jiji la Arusha ili kuhakikisha wanaendelea kulitangaza vyema Jiji la Arusha pamoja na kutoa hamasa kwa jamii kuhifadhi na kutunza mazingira kwenye vyanzo vya maji vinavyolizunguka Jiji hilo.
"Niendelee kuwasihi wadau wa utalii katika Jiji letu sambamba na wananchi wote waendelee kushirikiana na Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha wanatekeleza mipango ya kuimarisha shughuli za uhifadhi na utunzaji wa vyanzo vya maji". Alisema Iraghe
Sambamba na hilo ameendelea kuwakumbusha wananchi wa Jiji la Arusha kuwa asilimia 45 ya wagonjwa wanaotibiwa katika hospitali zilizopo ndani ya Jiji hili ni wenye magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo moyo, kisukari na kwamba njia mojawapo ya kuzuia matatizo hayo ni kufanya mazoezi.
Post A Comment: