Na. Damian Kunambi, Njombe.


Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Victoria Mwanziva amewataka viongozi wa ngazi zote Wilaya humo ikiwemo wakuu wa Idara kuhakikisha wanasimamia vyema fedha za miradi ya maendeo zinazoletwa na serikali katika maeneo yao na kuhakikisha fedha hizo zinaendana na ubora wa miradi hiyo.

Mwanziva ametoa maagizo hayo wakati alitoa hotuba katika kikao cha baraza la Madiwani cha robo ya 4 ya mwaka 2023/2024 na kusema kuwa hivi karibuni alifanya ziara ya kushtukiza ya kukagua utekelezaji wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya Maji na vyoo.

Ameongeza kuwa zkatika zahanati katika zahanati nne za kijiji Cha Luilo, Mbwila, Mawengi na Manga ambapo kila zahanati ilipewa fedha kiasi Cha Sh. Mil. 40 lakini baadhi yake zilitekeleza miradi hiyo vyema huku nyingine zikionesha mapungufu mbalimbali na hasa katika suala la manunuzi.

" Kwanza kabisa niliponza tu ziara na nigundua kuwa kuna Mil. 78 kwaajili ya usimamizi wa ujenzi wa uboreshaji miundombinu ya Maji na vyoo kitu ambacho kilinipa mashaka na kupelekea kuitisha nyaraka ambazo zilionyesha katika kiasi hicho Cha fedha zimesalia Sh. Mil. 21 pekee". Amesema Mwanziva.

Aidha ameongeza kuwa mapungufu mengine aliyokutana nayo ni katika manunuzi ambapo mfuko mmoja wa saruji ambao Ludewa hununuliwa kwa Sh. 18,000 Hadi 20,000 umenunuliwa kwa Sh. 30,000, Tanki la maji la Lita 5,000 ambalo huuzwa Sh. 900,000 limenunuliwa kwa Sh. Mil. 1.5, frem moja ya mlango wa kawaida umenunuliwa kwa Sh. 365,000 badala ya Sh. 150,000 sambamba na vitu vinginevyo kama makufuli na masinki ya vyooo.

Amesema hawezi kuuvumilia hali hiyo kwani serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inafanya jitihada kubwa sana za kuhakikisha kuwa inatekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi lakini Kuna watu wasiopenda maendeo na walio kuja serikalini kufuata ajira badala ya kazi hivyo hatomfumbia macho Mtumishi yeyote wa aina hiyo.

" Watumishi msiichukulie Ludewa ni pango la kujifichia wezi, serikali imekupa nafasi uliyonayo Ili ufanye kazi na si kuja kupata ajira tuu, watu mnajali shughuli zenu binafsi kuliko hata shughuli ambazo mmeajiliwa kuzifanya sasa kuanzia sasa naomba kuwataarifu kuwa hayo mambo si kwa Ludewa hii inayoiongoza mimi! nitahakikisha kila anayeenda tofauti anachukuliwa hatua stahili za kisheria".

Hata hivyo amesema imezoeeleka kuwa watumishi wanapofanya uharibifu wa kazi ikiwemo ubadhilifu huaamishwa kituo cha kazi hivyo katika Wilaya ya Ludewa hataki kuona mtu wa aina hiyo akihamishwa badala yake afukuzwe kabisa kazi kwani mtaani bado kuna watu wengi wanaohitaji ajira hivyo watapewa nafasi hao na kufanya kazi kwa ufanisi.

Ameongeza kuwa kumuhamisha mtumishi katika kituo kimoja kwenda kingine haisaidii kitu zaidi ya kumpa nafasi ya yeye kuendelea kuharibu katika eneo jingine tena na hakuwezi kumfunza chochote.

Hata hivyo kwa upande wao Madiwani wamepokea kwa masikitiko taarifa hizo huku wakimpongeza mkuu wa Wilaya kwa kufanya kazi kwa uhodari akiwemo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Wise Mgina ambaye amesema katika zoezi la ukaguzi wao wa miradi walifika baadhi ya maeneo na kuambiwa kuwa mkuu huyo wa Wilaya alipita na walipohitaji nyaraka za miradi waliambiwa zimechukuliwa.






Share To:

Post A Comment: