Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa -TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa katika ujenzi wa shule ni uhimarishaji na ujenzi wa miundombinu ya msingi inayowezesha kuongeza nafasi za udahili wa wanafunzi katika shule mbalimbali.
Mhe. Katimba amesema licha ya Serikali kutambua uhitaji mkubwa wa ujenzi wa uzio kwa ajili ya ulinzi na usalama wa mali za shule na wanafunzi wa bweni, lakini kwa sasa imejikita zaidi kwenye udahili wa wanafunzi ili kuwawezesha kuanza masomo.
Mhe.Katimba ameyasema hayo leo (Agosti 28,2024) Bungeni Jijini Dodoma katika kipindi cha Maswali na Majibu wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mhe. Ally Juma aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupeleka fedha za ujenzi wa uzio wa Shule ya Wasichana Kondoa ili kuimarisha ulinzi na usalama wa wanafunzi.
Amesema kwa mwaka wa fedha 2021/22 na 2023/24 Serikali kuu imepeleka zaidi ya shilingi milioni 600 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ikiwemo Vyumba vya Madarasa 8, Mabweni 2, Matundu ya vyoo 14 na Vitanda 660 katika Shule ya Wasichana Kondoa kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Post A Comment: