📌Ajira kwa Watanzania kupewa kipaumbele

📌 Ni Mradi wa Dola Milioni 77 kwa Maendeleo ya Viwanda Nchini

📌 Utafiti Waonesha Uwepo wa Tani Milioni 101 za Chuma

📌 Dkt. Biteko Ahimiza Wananjombe Kutumia Fursa za Mradi 


Tanzania imeandika historia mpya ya matumizi ya rasilimali zake kufuatia kusainiwa kwa utekelezaji wa mradi wa uchimbaji wa chuma wenye thamani ya dola milioni 77.

Mradi huo ambao utatekelezwa katika eneo la Maganga Matitu Wilayani Njombe unatarajiwa kuchochea maendeleo ya viwanda nchini na hivyo kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumza Agosti 2, 2024 mkoani Njombe  mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mkataba wa Uchimbaji Madini ya Chuma Maganga Matitu kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa NDC na Kampuni ya Fujian Hexingwang Industry Tanzania .Co.Ltd. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema mafanikio hayo yametokana na jitihada za Serikali kuchochea matumizi sahihi ya rasilimali kwa manufaa ya Watanzania.











Share To:

Post A Comment: