Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za nishati na maji (EWURA CCC) leo Agosti 4,2024 imeendelea kutoa elimu katika maonesho ya Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Nzunguni Jijini Dodoma.

Katika elimu hiyo iliyoitoa kwa baadhi ya Wananchi waliotembelea katika banda hilo ni pamoja na kazi inazozifanya na wajibu wa mtumiaji wa huduma za maji na nishati anapaswa kufuata ili kupata haki yake ya msingi kama mteja.

Baadhi ya Wananchi waliotembelea katika banda la EWURA CCC wameonekana kufurahishwa na kazi wanayofanya katika kuhakikisha wanawatetea ili kupata haki zao za msingi.


"Tuna mfurahi sana kwa kile mnachokifanya kwasababu tulikuwa hatujui wapi tupeleke malalamiko yetu unakuta kila siku tunalia hasa kwenye upande wa maji lakini kwakuwa sasa tumeshapata elimu na kujua wajibu wetu ni upi hivyo zile changamoto zetu zitaenda kutatuliwa sasa",wamesema.

Baraza la Ushauri la watumiaji wa huduma za maji na nishati lilianzishwa chini ya kufungu cha 30 cha sheria ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za Nishati na maji , sura ya 414.

Lengo la Baraza hilo ni kutetea na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma za maji na nishati ambazo ni majisafi na majitaka, umeme, petroli na gesi asilia.


Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: