Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), akizungumza na Viongozi mbalimbali wa Benki ya Dunia, na Baadhi ya Mawaziri wa Fedha wa nchi za Afrika, wakati wa Mikutano ya Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu kutoka nchi za Afrika (Africa Caucus Meetings), Nchi wanachama wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, unaofanyika katika Hoteli ya Transcorp Hilton, mjini Abuja Nchini Naigeria.

Miongoni mwa Viongozi hao ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, Bi. Viktoria Kwakwa, na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko.

Wegine ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Sudan, Mhe. Dkt. Gabriel Ibrahim Mohamed na Waziri wa Fedha na Maendeleo ya Kiuchumi wa Uganda, Bw. Amos Lugoloobi na pia aliteta jambon a Katibu Mkuu ambaye pia Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali Dkt. Natu El-maamry Mwamba.

Share To:

Post A Comment: