MSIMU wa tatu wa mbio za mabadiliko ya tabianchi 'Climate Change Marathon kwa mwaka 2024 zinatarajiwa kufanyika wilayani Pangani kwa mara ya  kwanza zikihusisha washiriki kutoka ndani na nje ya mipaka ya Tanzania zikilenga kukusanya fedha zitakazotumika kugawa majiko ya gesi ya kupikia kwa wanawake ikiwa ni agenda ya kitaifa kuondokana na matumizi ya Kuni na mkaa.

Wanufaika katika mbio hizo ambao ni wanawake kutoka katika wilaya za  Pangani  na Handen Mkoani Tanga  hususani waliopo katika Kijiji cha  Msomera ambao walihama kutoka hifadhi ya Taifa Ngorongoro zikiandaliwa  na taasisi ya Tree of Hope kwa kushirikiana na   asasi ya Muungano wa jinsia na mabadiliko ya tabianchi.

Akizungumza mkurugenzi wa Tree of Hope Fotunata Fortunate Manyeresa  alisema mbio hizo zitafanyika September 28,2024 zikitanguliwa na bonanza la michezo mbalimbali ambapo pia  washiriki watapata fursa ya kutembelea Mbunga ya za wanyama  Saadani huku zaidi ya kaya 50 zikitarajiwa kunufaika mpango huo.

"Mbio za mabadiliko ya tabianchi kwa mwaka 2024 zinalenga kukusanya fedha  kwa ajili ya kuhamasisha jamii kutumia nishati mbadala ili kuwasaidia wanawake katika wilaya za Pangani na Handeni waliopo Kijiji cha  Msomera na tunategemea zaidi ya kaya 50 zitanufaika, mpango huu unalenga pia kupunguza uchafuzi wa mazingira  tunatarajia kwamba tukio hili litaongeza uelewa kwa jamii juu ya athari za mabadiliko ya tabia nchi" alisema Manyeresa.

Mathias Lyamunda ambaye ni mkurugenzi  kutoka mtandao wa FEMAPO alisema mbio hizo zitajumuisha Kilomita 21 mshindi akiondoka na kitita  cha shilingi 500,000, Kilomita 10 atakayezawadiwa shilingi  300,000  ,Kilomita 5 (250,000) pamoja na Kilomita 2.5 ambapo kila mshiriki atanakiwa kuthibitisha ushiriki wake kwa gharama ya shilingi elfu 35, na kwa watoto ni elfu 10,000.

Katibu wa chama cha riadha Mkoa wa Tanga  Hassan Mwagomba  wametoa baraka zote kwa taasisi hiyo ya Tree of Hope  akiwakaribisha wadau wengine kushirikiana nao katika kuunga mkono jitihada mbalimbali za Serikali katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kwa jamii pamoja na utunzaji wa mazingira.

Share To:

Post A Comment: