Zadi ya wakazi Elfu Tatu miatano wamitaa Minne ya Miembeni,Idara ya Maji Kiliman pamoja na Butakale Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wameanza kunufaika na Upanuzi wa Mtandao wa Maji baada ya kukosa maji kwa Muda mrefu.

Maeneo ya mitaa hiyo yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya ukosefu wa Maji ambapo Mamlaka ya Maji Safi na usafi wa Mazingira (BUWASA) wameanza kuongeza mtandao wa maji kwa maeneo hayo.

Changamoto ya ukosefu wa Maji ya Muda mrefu katika mitaa Saba ya Miembeni,idara ya Maji Kiliman, Butakale imepata ufumbuzi baada ya kuanza Upanuzi wa Mtandao wa Maji  kwa wakazi wa mitaa hiyo.

Akizungumzia hali hiyo Mkurugenzi wa Maji Safi na usafi wa Mazingira(BUWASA) Ester Gilyoma amesema Serikali inahakikisha wananchi wake wananufaika na Mradi huo wa Maji na sasa mtandao huo utawafikia wakazi takribani 3500 katika mitaa minne Halmashauri ya Mji wa Bunda.

Utekelezaji wa mradi huo wa maji adhima ya DK Samia Suluhu Hassan kumtua mama ndio kichwani kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa Maji inaondolewa.

Share To:

Post A Comment: