Wizara ya Madini imeendelea na Kliniki ya Madini katika Mkoa wa Songwe katika ngazi ya Wilaya, Kata na Vijiji kwa lengo la kupokea kero na changamoto za wachimbaji wadogo wa madini.

Julai 4 , 2024 Naibu Waziri wa Madini  Dkt.Steven Kiruswa wilayani Momba alikutana na wachimbaji wadogo wa madini na kuzungumza nao kwa lengo la kujua changamoto zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.

Akiwa katika kijiji cha Chindi , Kata ya Msangano, Naibu Waziri  Dkt. Kiruswa alitembelea Mgodi wa mchimbaji mdogo wa Madini ya Sodalite na kupokea taarifa ya maendeleo ambapo mpaka sasa mgodi huo umezalisha kiasi cha  tani 50  huku changamoto kubwa ikibainishwa ni ukosefu wa mtaji , kutokuwepo kwa mthaminishaji wa madini katika  eneo la uzalishaji, soko la uhakika na ubovu wa miundombinu.

Sambamba na madini hayo ,  Dkt.Kiruswa alikutana  na wachimbaji wa Gesi ya Helium na  Madini ya Chumvi ambapo katika miradi hiyo  aliwapongeza kwa juhudi mbalimbali wanazofanya katika kuendeleza miradi hiyo ambayo ni muhimu katika sekta ya uchumi nchini.

Naye , mbunge wa Jimbo la  Momba, Condester Sichalee  aliishukuru Wizara ya Madini kwa kuanza kuendesha kliniki ya madini katika mkoa wa Songwe na kupokea changamoto mbalimbali ambazo zikitatuliwa itakuwa faida kubwa kwa wachimbaji wa mkoa huo na kuendeleza sekta ya madini mkoani wilayani Momba.

Julai 4, 2024,Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa amehitimisha ziara yake maalum ya Kiliniki ya madini mkoani Songwe.



Share To:

Post A Comment: