1000370083

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Silaa (Mb) leo tarehe 30 Julai, 2024, ametembelea ofisi za makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) zilizoko jijini Dar es Salaam na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe.

Waziri Silaa amefanya ziara hiyo kwa lengo la kujifunza na kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo na namna wanavyoshughulikia masuala ya Habari na Mawasiliano.

Katika ziara hiyo, Waziri Silaa ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Bw. Nicholas Merinyo Mkapa pamoja na Maafisa Waandamizi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
1000370077
1000370080
10003700861000370092
Share To:

Post A Comment: