Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akikabidhi mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ramani baada ya matokeo ya Sensa
Waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Majaliwa akisalimiana na viongozi mbalimbali katika viwanja vya Kilomahewa




Na Fredy Mgunda, Lindi.

WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa serikali kutumia vizuri takwimu za serikali kupanga mipango ya kimaendeleo katika Halmashauri mbalimbali.

Akizungumza wakati wa mafunzo ya usambazaji na matumizi ya matokeo ya Sensa viongozi, watendaji na makundi mbalimbali kutoka wilaya ya Nachingwea, Ruangwa na Liwale,Waziri mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa alisema kuwa sasa takwimu za kila eneo zimajulika hivyo ni jukumu la viongozi kutumia vizuri takwimu hizo kupanga mipango madhubuti.

Majaliwa alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kupeleka maendeleo kulingana na idadi ya wananchi waliopo eneo husika, ukubwa wa eneo,mateja wapo wangapi.

Aliongeza kuwa madiwani wote wanatakiwa kutumia matokeo ya Sensa kuleta maendeleo kwa wananchi kwenye kata zao hivyo viongozi wote mkitumia matokeo ya takwimu hizo basi itakuwa kazi rahisi kupeleka maendeleo kwa wananchi.

Waziri mkuu Majaliwa aliongeza kuwa hata taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kutumia takwimu hizo za serikali kupanga mipango madhubuti ya kimaendeleo kwa kuwa zinaonyesha dira ya maendeleo.

Ukiwa na takwimu hizo za Sensa zinasaidia kwenye biashara,kilimo,afya na kutoa miongozo mbalimbali ya kuongeza ufanisi wa kutekeleza majukumu ya kiungozi na utumishi
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: