Wakazi wa vijiji vya matongo,mjini kati pamoja na ya Matongo iliyopo Nyamongo wilayani Tarime mkoani Mara wameondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya maji baada ya kukamilika kwa mradi maji uliojengwa na Mgodi wa Barrick North Mara kwa kushirikiana na Serikali.
Kufuatia hali hiyo wameishukuru Serikali na mgodi kwa ujenzi wa mradi huo uliogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 1, kwani hapo awali walizamika kutumia muda mwingi kutafuta huduma katika visima na mito iliyo mbali na makazi yao.
wananchi walienda mbali nakusema kuwa kipindi cha nyuma wamekuwa wakilazimika kununua maji ndoo kiasi cha shilingi 3500 kwa wauzaji wa baiskeli hali ambayo ilikuwa inawapa ugumu nakulazimika kuchota maji kwenye mito.
''Sasahivi hatuna mawazo kabisa ya maji ile eti uamke usiku asubuhi unawahiwahi hapana sahivi nikunywa maji nikiwa ndani naamka muda ninaotaka labda niamke kufanya shughuli zingine mgodi umetusaidia sana'' Alisema Stela lukasi mkazi wa nyamongo.
Awali akizungumzia mradi huo msimamizi wa chombo cha watoa huduma wa maji nyamongo Ayubu Mrwafu alisema mradi wa maji umekuwa msaada mkubwa katika eneo hilo kutokana na eneo hilo lilikuwa changamoto kubwa ya ukosefu wa maji ambapo kukamilika kwa mradi huo umekuwa msaada mkubwa kwani awali mgodi ulikuwa unasambaza maji kwa boza na sasa wananchi wamefikishiwa huduma hiyo nyumbani.
''wananchi walikuwa wananunua maji kwa shilingi 3500-hadi 4000 na wakati mwingine walikuwa wakitegemea boza kutoka mgodini ambalo lilikuwa linasambaza maji kwa wananchi lakini sasa baada ya serikali kushirfikiana na mgodi kuleta wazo lakutatua hii changamoto ndio wakaanzisha mradi huu kupitia fedha za huduma za jamii kwa mwaka 2021-2023 mradi ukakamilika na tukakmabidhiwa mradi mwezi wa 7 ukiwa na vituo 20 vya kuchotea maji''Alisema Ayubu msimamizi wa chombo cha watoa huduma wa maji.
Aidha baadhi ya wenyeviti wa vijiji wamekili kusema kuwa kwa sasa adha ya maji imepungua kutokana na kuendelea kusambazwa kwa mtandao wa maji ambapo kwa sasa mradi huo unahudumia vijiji vinne vya kata ya matongo.
Post A Comment: