Umoja wa vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM (UVCCM) umeandaa kampeni maalum ya kitaifa itakayo fanyika Julai 6, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa (LUPASO) jijini Dar es Salaam yenye lengo la kuwahamasisha vijana kushiriki katika Maswala ya kisiasa.

Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo, amesema uzinduzi wa kampeni hiyo muhimu umelenga kuwakutanisha vijana na kujadili fursa muhimu zilizotengenezwa na serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan. 

Aidha, Jokate ametoa wito kwa vijana kushiriki kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa serikali za mtaa sanjari na kuwataka watu wote kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura litakalo zinduliwa julai 20 mwaka huu katika mkoa wa Kigoma.




Share To:

Post A Comment: