Mbunge wa jimbo la Chalinze na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe.Ridhiwani Kikwete leo Amefanya ziara katika kata ya Mkange, kutembelea Vikundi vya Wananchi na pia kufanya mkutano mkuu wa kata ya mkange.

Hata hivyo amekagua vikundi ambavyo viliidhinishwa na Mhe Dkt. Samia kwaajili ya kupata mkopo wa asilimia kumi

Lakini pia Mhe. Ridhiwani Kikwete amewasisitiza wananchi kuhusu uandikishaji wa kadi za kupiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa vijiji na vitongoji pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.






Share To:

Post A Comment: