Na Denis Chambi, Tanga.


MKUU  wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt. Batilda Buriani amewataka wakuu wa wilaya za mkoa huo  kufanya ukaguzi wa mifumo ya  ukusanyaji wa mapato  kila baada ya wiki  katika halmashauri zao ili kuziba mianya yote ya upotevu wa fedha za Serikali zinazopatikana kupitia vyanzo mbalimbali.

Mkoa wa Tanga katika mwaka wa fedha 2022/2023 umeweza kuvuka lengo la kusanyaji wa mapato na hatimaye kifikisha asilimia 104  ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo Wilaya ya Kilindi ikiwa Kinara katika halmashauri 9 za mkoa huo baada ya kukusanya kwa asilimia 131. 

Balozi Buriani ametoa maagizo hayo July 16,2024 wakati  akikabidhi Magari mapya manne kwa wakuu wa wilaya za Kilindi, Pangani, Korogwe  na  lingine moja kwajili ya ufwatiliaji wa miradi ya maendeleo yaliyoghalimu kiasi cha shilingi Milion 683 ambapo amewataka yakawe chachu ya kuongeza utendaji  kazi wao,  kutatua kero za wananchi sambamba na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama.

"Niendelee kuwapongeza sana kama mkoa tumeweza kufanikiwa kukusanya mapato ya takribani asilimia 104  haijawahi kutokea mkoa wetu  kufikia kiwango hicho inaonyesha halmashauri zetu 5 zimekusanya na kuvuka lengo la asilimia 100 halmashauri zingine tunajua wanao uwezo wakaze buti wahakikishe wanasimamia wakusanyaji wa mapato "alisema But Buriani

"Na uzuri tunao mfumo unaoonyesha wanaokusanya mapato fedha zinazobaki mikononi ambazo haziwekwi kwenye akaunti za benki kama ambavyo inatakikana  wakuu wa wilaya kila wiki mpite kwenye halmashauri mdai wakurugenzi wawape taarifa za mifumo muweze kujua fedha zinazokusanywa na ambazo ziko mikononi mjue ni kiasi gani tumekusanya na kipi hatujakusanya"alisisitiza 

"Tunategemea kuwaona mkiwatembelea wananchi msikilize na kutatua shida zao  na kuona jinsi ya kuzitatua , tusaidie katika kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo yetu lakini zaidi kuwasaidia wananchi katika kuhakikisha juhudi za kujileta  maendeleo zinafanikiwa".

Aidha Dkt Buriani amepongeza ufaulu mzuri katika matokeo ya kidato cha sita mwaka ya  2024  ambapo Mkoa umefanikiwa kutinga nafasi ya 10 Bora kupitia shule ya Sekondari Mkindi  iliyopo wilayani Kilindi ambayo imetoa wanafunzi bora 7 wa kike akiwataka wakuu wa wilaya kuongeza usimamizi na ufuatiliaji katika sekta ya elimu ili kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinazidi kuongezeka.

"Kipekee nawapongeza sana kwa matokeo mazuri ya kidato cha sita mkoa umefanya vizuri katika 10 bora shule yetu ya Mkindi Sekondari ipo na katika wanafunzi bora wa kike tunao wanafunzi zaidi ya  7  wapo katika kikundi kile cha 10 bora kwahiyo tujitahidi" alisema Bkt Buriani na kuongeza ..

'"Huu ni mkoa ambao elimu ilianza  hakuna sababu ya kuwa chini hapa tulipofika nina imani tunaweza kuwa na matokeo mazuri zaidi kwaajili ya kuendelea historia ya mkoa wetu wa Tanga"

Akizungumza Mwenyekiti wa wakuu wa wilaya za mkoa wa Tanga ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Kilindi Hashimu Mgandilwa amesema  ujio wa Magari hayo umeowaongezea ari ya utendaji kazi ambao itakwenda kutimiza adhima ya Serikali katika nyanja mbalimbali husausani kuwafikia wananchi kwa kutatua kero zao na kuwaleta maendeleo.

" Kwa niaba ya wenzangu niendelee kumpongeza na kumshukuru sana Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutukabidhi vitendea kazi hivi, tukuhakikishie vyombo hivi vya usafiri tutakwenda kuvitumia  vizuri katika yale matarajio ambayo yeye binafsi anapenda yatokee kwa wananchi wetu hususani utatuzi wa migogoro na usimamizi wa miradi  vitendea kazi hivi vimetutia chachu na kutuongezea ari ya ufanyaji wa kazi"alisema Mgandilwa.

Katibu wa chama cha Mapinduzi 'CCM' mkoa wa Tanga Suleimani Sankwa amepongeza utendaji wa watumishi  wote waliopo chini ya mkuu wa mkoa kwa kazi wanazoendelea kuzifanyia kwa kutimiza majukumu yao ipasavyo ambayo imeongeza na kuchagiza maendeleo kuanzia ngazi ya vijiji na vitongoji na mitaa.

Share To:

Post A Comment: