Na. James K. Mwanamyoto OR-TAMISEMI
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba amesema, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa milioni 105 zilizoboresha miundombinu ya Shule ya Msingi Mvinza na milioni 365.5 zilizojenga shule mpya ya Msingi ya Songambele ambayo imepunguza msongamano wa wanafunzi uliokuwepo katika shule ya Mvinza wilayani Kasulu.
Mhe. Katimba amesema hayo, wakati akizungumza na wananchi wa Mvinza wilayani Kasulu alipoitembelea shule ya Mvinza kwa ajili ya kukagua uimara wa miumbombinu iliyoboresha kwa fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuona kupitia mitandao ya kijamii changamoto ya msongamano wa wanafunzi iliyokuwa ikiwakabili wanafunzi wa shule hiyo.
Mhe. Katimba amesema, utekelezaji wa sera ya elimu bure ya kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha sita ndio iliibua changamoto hiyo ya msongamano wa wanafunzi ambayo iliyovuma katika mitandao ya kijamii hivyo Mhe. Rais akatoa fedha kiasi cha shilingi milioni 470.5 kutatua changamoto hiyo.
“Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alisikia kilio chenu na akashusha fedha milioni 105 katika kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Shule ya Mvinza na milioni 365.5 za kujenga shule mpya ya Msingi ya Songambele,” Mhe. Katimba amesitiza.
Mhe. Katimba ameongeza kuwa, katika shule ya Songambele fedha hizo zimewezesha kujenga madarasa 7 na tayari imeshapokea wanafunzi 923 ikiwa ni pamoja na kujenga shule ya awali inayosaidia kujenga msingi imara wa makuzi ya watoto pamoja na kuwaanda kuingia darasa la kwanza.
Aidha, Mhe. Katimba ametoa maelekezo kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuwataka wasimamizi wa ujenzi wa miundombinu ya elimumsingi kuzingatia ubora na miongozo inayotolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI ili kufikia azma ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaendelea kutekeleza azma yake ya kuboresha miundombinu ya elimumsingi nchini, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya mwaka 2020/25 ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akizungumza na wananchi wa Kata ya Makere (hawapo pichani) mara baada ya kukagua miundombinu ya Shule ya Msingi Makere iliyopo Wilayani Kasulu, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Makere wilayani Kasulu wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba (hayupo pichani) mara baada ya Naibu Waziri huyo kukagua miundombinu ya Shule ya Makere ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akitoka kukagua miundombinu ya darasa la awali katika Shule ya Msingi Makere, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akizungumza na wananchi wa kijiji cha Maviza Wilayani Kasulu, mara baada ya Naibu Waziri huyo kukagua miundombinu ya shule ya Msingi Maviza.
Mwonekano wa baadhi ya mejengo yaliyopo katika Shule ya Msingi Songambele Wilayani Kasulu, ambayo yamejengwa kwa fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Maviza Wilayani Kasulu, wakisikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba, mara baada ya Naibu Waziri huyo kukagua miundombinu ya Shule ya Msingi Maviza.
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (Elimu) Mhe. Zainab Katimba akikemea tabia ya walimu wa Shule ya Msingi Songambele Wilayani Kasulu ya kutelekeza ofisini vitabu vilivyoletwa na Serikali kwa ajili ya kuwapatia watoto wa elimu ya awali.
Post A Comment: