Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amekabidhi jengo la Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Dkt. Tausi Kida ili kuendelea na utekelezaji wa Mradi huo.
Hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika leo Julai 17,2024 katika Mji wa serikali Mtumba jijini Dodoma ambapo awali mradi wa ujenzi wa jengo hilo ulikuwa ukisimamiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) kabla ya kuundwa kwa Wizara ya Mipango na Uwekezaji ambayo ipo Chini ya Ofisi ya Rais.
Post A Comment: