Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2024 Godfrey Eliakimu Mnzava amezitaka Taasisi za serikali pamoja na mashirika ya umma kutumia mfumo wa  kieletroniki wa  NeST kwaajili ya manunuzi ili kudhibiti mianya ya  rushwa  pamoja na kuondoa upendeleo katika zabuni zinazotolewa ili kuhakikisha miradi inayojengwa inazingatia ubora.

Mnzava ametoa agizo hilo wakati wa ukaguzi wa barabara ya boksi kalavati Mbuguni,Shambarai Burka iliyojengwa kwa gharama  ya sh,milioni 99.499 na  Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA).

Alisema endapo mfuko huo ukitumiwa  vema utapunguza masuala ya rushwa ikiwemo upendeleo wa zabuni na kazi  zinazotolewa hususan za ujenzi ikiwemo upendeleo kwenye miradi kwa Watu wasio na sifa za ujenzi.

"Tumieni mfumo wa NeST kwaajili ya manunuzi lakini pia mfumo huo utadhibiti rushwa haswa katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo"

Awali Mhandisi wa TARURA wilaya ya Arumeru,Julius Kaaya alisema kalavati hilo lenye urefu wa kimolita 7.9 linunganisha kata hizo kwaajili ya kurahisisha huduma za usafiri na usafirishaji wa mazao kutoka shambani hadi sokoni.

Alisema kazi zilizofanyika ni Kuta za Daraja pamoja na masikio yake,deku ya Daraja na sehemu ya relief za vizuizi na Daraja hili limejengwa na makandarasi wa kampuni ya Lenana Holding Company Limited 

Wakati huo huo,baadhi ya wananchi wa Shambarai Burka akiwemo ,Mariam Zakaria alishukuru daraja hilo kujengwa kwani Awali wananchi hao walikuwa wakikabiliwa na changamoto ya barabara kujaa maji kutokana na ukosefu wa daraja na kuomba barabara hiyo kutengenezwa zaidi ili kuondoa changamoto ya vumbi.

"Ujenzi wa daraja hili utarahisisha bidhaa zetu kutoka shambani kwenda soko la Mbuguni na masoko mengivkwa haraka zaidi ikiwemo kijikwamua kiuchumi, tunamshukuru sana Rais Samia Hassan Suluhu kwa kwa barabara hii "

Mwenge wa uhuru umewasili rasmi  Mkoani Arusha ulitokea Mkoani Manyara  ambapo utakimbia  kilomita 1182.9 na kukagua miradi 65 yenye thamani ya sh,bilioni 61.6

Awali  mwenge huo wa uhuru ulipokelewa  katika kijiji cha Migungani kata ya Mbuguni Wilayani Arumeru na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Nurdin Babu  ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro amesema mwenge huo utazindua miradi hiyo Mkoani Arusha 

Mwenge huo wenye wenye kauli mbiu ya " Tunza mazingira na shiriki uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ujenzi wa taifa endelevu"






















Share To:

Post A Comment: