Katibu Mkuu, Ofisini ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Mary Maganga akizungumza na watumishi wa ofisi ya CMA kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara kushoto ni Mkurugenzi wa CMA Usekelege Mpulla yaliyofanyika leo Jijini Dodoma. 

Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) akizungumza na watumishi wa ofisi ya CMA kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya mfumo wa kusajili migogoro ya kikazi unaofahamika kama ‘Online Case Management’ kwa watumishi wa Tume hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dodoma. 

Watumishi wa ofisi ya CMA kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya mfumo wa kusajili migogoro ya kikazi unaofahamika kama ‘Online Case Management’ kwa watumishi wa Tume hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dodoma. 

Matukio ya picha za pamoja kutoka kwa Watumishi wa ofisi ya CMA kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum ya mfumo wa kusajili migogoro ya kikazi unaofahamika kama ‘Online Case Management’ kwa watumishi wa Tume hiyo yaliyofanyika leo Jijini Dodoma. 


Na Mwandishi Wetu, Dodoma.


Katibu Mkuu, Ofisini ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Mary Maganga amesema mfumo mpya wa kusajili migogoro ya kikazi kwa njia ya mtandao utaepusha malalamiko na ucheleweshwaji wa haki kwa Wananchi ikiwa ni Pamoja na kuongeza ufanisi wa utendaji wa Tume.


Mhe. Maganga ameyasema hayo leo,Julai 24,2024 Jijini Dodoma, wakati akifungua mafunzo maalum ya mfumo wa kusajili migogoro ya kikazi unaofahamika kama ‘Online Case Management’ kwa watumishi wa CMA kutoka Ofisi mbalimbali za mikoa Tanzania.


Vilevile Mhe. Maganga ameongeza kuwa,matumizi ya mifumo yanaongeza ufanisi wa utendaji kwa namna mbalimbali na pia uwezo wa kutumika katika mazingira mbalimbali bila kuhitaji kwenda katika ofisi husika kupata huduma.


"Mara nyingi tukiwa tunataka kuongeza ufanisi pa kwenda ni kwenye mifumo kwasababu mifumo unaweza kuitumia popote pale ulipo na bila kuhitaji kwenda kwa uhalisia kwahiyo tuna imani kubwa itaenda kuongeza ufanisi wa Tume yetu", amesema Mhe. Maganga.


Aidha Mhe. maganga amewataka watumishi kuendelea kusimamia haki katika ajira na kazi kwa kuhakikisha wanatatua migogoro kwa njia ya usuluhishi kwani ndio wajimu wao kwa Tume.


Vilevile ameipoingeza Tume kwa kuendelea kusuluhisha migogoro ya kikazi hadi kufikia asilimia 76% ikiwa ni hatua nzuri kulingana na mpango mpango wa kuhakikisha wanafikia asilimia 81% kwa njia ya Usuluhishina hivyo kuonekana katika hatua inayoridhisha.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Mhe. Usekelege Mpulla amesema mfumo huu unatarajiwa kutumika kutekeleza lengo la Tume ikiwa ni kuwafikia wadau mbalimbali kwa urahisi popote walipo.


"Kwa msingi huo tunatarajia kupitia mfumo huu tuweze kuwafikia wadau wetu na kusajili migogoro kwa kutumia, simu janja ili nasi tuweze kuishughulikia kwa haraka maana hili ni takwa na ombi la muda mrefu la wadau wetu hasa wawekezaji kutaka huduma za Tume ziende kwa haraka", ameongeza mkurugenzi.


Naye Afisa Mfawidhi kutoka Ofisi ya CMA Arusha, Hermenegilda Stanslaus alisema mfumo huo utawasaidia watumishi wa Tume katika kutekeleza majukumu na kurahisisha utendaji kazi bila kuwalazimu wateja na wadau mbalimbali kufika ofisi za Tume.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: