KATIKA kufanikisha mkakati wake wa kufanikisha usambazaji wa nishati ya jua nchini na bidhaa bora zinazotumia nishati hiyo, kampuni ya Sun King imefungua ofisi zake mkoani Arusha.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hizo ulihudhuriwa na Makamu wa Rais wa Mauzo wa Sun King, Victor Agandi, Meya wa Jiji la Arusha, Mhe. Maximilian Iranghe na wageni mbalimbali.

Meya Iranghe, aliipongeza Sun King kwa kujitolea kwa jamii, kwa kutoa mtambo wa kisasa wa umeme wa jua (Solar Inverter) sambamba na kuadhimisha uzinduzi.Mtambo huo wa kusambaza umeme wa jua wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 7,000,000 uliofungwa utawezesha maabara ya kituo cha afya cha Themi kilichopo jijini Arusha kufanya kazi na kusambaza umeme kwenye wodi ya akina mama, na hivyo kuimarisha utendaji kazi wa kituo hicho na jamii kupata huduma bora za afya.

Mfumo huu wa kibunifu wa umeme jua, ni mojawapo ya bidhaa za hivi karibuni za Sun King, umeundwa kushughulikia matatizo mengi ya nishati hapa nchini Tanzania. Tunaahidi kuendelea kupunguza gharama kubwa za nishati kuanzia kwenye kaya za mijini na biashara kwa ujumla.

"Ninayo furaha kusikia kwamba Sun King hivi karibuni ilitunukiwa Tuzo ya Kampuni Bora ya Mwaka ya Watoa huduma za Bidhaa za umeme wa jua katika Tuzo za Kampuni Bora ya Afrika," alisema Meya Iranghe. "Sifa hii inadhihirisha kuwa mnavyo vigezo vya kutoa huduma zenu nchini na Afrikai, ikithibitisha dhamira ya Sun King ya kusaidia kuleta maisha bora kwa mamilioni ya watu ulimwenguni kote."

Akitoa shukrani zake kwa wageni na wafanyakazi wa Sun King Tanzania, Victor Agandi, Makamu wa Rais Mauzo ya huduma za Nishati ya jua kwa mfumo wa gharama nafuu kwa wateja kwa Afrika Mashariki na Kusini, alisema, "Hili ni tukio muhimu kwa Sun King Tanzania. Ninajivunia mafanikio yetu na ninashukuru kwa matokeo chanya tuliyoleta Tanzania na Afrika kwa ujumla. Tunaendelea kuwa thabiti katika dhamira yetu ya kutoa suluhisho la nishati ya jua kwa bei nafuu, kuaminika na endelevu kwa wale walengwa.

Kujitolea kwa Sun King kwenye uvumbuzi na matokeo chanya kwenye kijamii kumeiweka kama kiongozi kwenye tasnia. Dhamira ya kampuni ya kuendelea kupeleka nishati safi kwa watanznaia ambapo mpaka sasa watanzania takribani milioni mbili wamefikiwa na nishati hii. Sun King inaendelea na safari yake ya kuleta matokeo chanya na bora, kukuza maendeleo endelevu na ustawi duniani kote. Kampuni imepata tuzo nyingi na sifa kwa ufumbuzi wake wa ubunifu kwa changamoto za upatikanaji wa nishati, ikiwa ni pamoja na kutambuliwa kutoka kwa Shirika la Fedha la Kimataifa, S & P Global Platts, tuzo ya Ashden na tuzo ya Global LEAP kwa kutaja chache.

Shughuli za Sun King zimesambaa katika nchi nyingi barani Afrika, zikiwemo Cameroon, Kenya, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Tanzania, Togo, Uganda, na Zambia. Sun King inatoa huduma zake kwa kushirikiana na wasambazaji wa ndani, taasisi ndogo za fedha, na mashirika yasiyo ya kiserikali katika nchini za Afrika ili kufikia jamii mbalimbali zisizounganishwa za gridi ya Taifa.









Share To:

Post A Comment: