MBUNGE wa Jimbo la Vunjo, Dkt. Charles Kimei amesikitishwa kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa mradi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya Sekondari ya Himo iliyopo kata ya Himo wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro.


Mbunge huyo alionyesha kusikitika huko mara baada ya kufika kutembelea shule hiyo ambapo alisema kuwa, changamoto ya kukamilika kwa mradi huo ni mkandarasi kuw na kazi zaidi ya moja hali ambayo inapelekea kushindwa kutawanya nguvu.


“kunalo tatizo kwa halmashauri yetu katika kuchambua zabuni kwani inawezekana Mkandarasi huyo anazo kazi nyingine hivyo inapelekea kushindwa kutawanya nguvu yake hivyo niwaombe Halmashauri iache tabia ya kumlumbikia mtu mmoja kazi nyingi” alisema Dkt. Kimei.

Mbunge huyo alisema kuwa, lazima kufanyike tathimini katika kuchambua zabuni ambapo ni wajibu kuangalia uwezo wa kifedha kwani mara nyingi wamekuwa hawapimi rekodi za wakandarasi hali inayopelekea miradi kuchelewa kukamilika.


Alisema kuwa, kwa sasa walimu wanajukumu la kusimamia mradi huo ambao kwa sasa unatumia force akaunti ambapo wanatumia mafundi wazawa na kuwataka kuhakikisha mradi huo unakamilika haraka ili lengo la serikali la kuleta mradi huo liweze kutimia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Himo Sekondari, Zailo Mhadisa alisema kuwa, shule hiyo ilipokea zaidi ya milioni 492 kwa ajili ya ujenzi wa majengo mapya ya kidato cha tano na sita kwa ajili ya Jengo la utawala, Bweni moja, Madarasa manne, maabara mbili na vyoo vya matundu 23.

Alisewa kuwa, mradi ulianza kutekelezwa Machi 6 mwaka huu na ulipaswa kukamilika Juni 6 mwaka huu ambapo Mkandarasi alishindwa kwenda kwa kasi inayotakiwa na mpango kazi uliokuwepo na kulazimika halmashauri kuvunja mkataba.




Share To:

Post A Comment: