MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ameshangazwa Mazingira machafu Mtaro wa maji ya Mvua Mtaa wa KIMANGA wilayani Ilala viongozi wa eneo hilo kushindwa kuchukua hatua.
Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alifanya ziara kata ya Kimanga leo wakati wa kukagua miradi ya maendeleo ambapo alifanya ziara Mtaa wa KIMANGA katika mradi wa mifereji na kukuta mfereji wa maji ya mvua mchafu ambapo alitoa agizo kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdalah Lumungwi jumamosi hii ashiriki usafi wa pamoja kusafisha mtaro pamoja na Mbunge.
"MWENYEKITI mtaro huu mchafu umeshindwa kuchukua hatua za kusafisha na wananchi wako Jumamosi nitakuja kushiriki usafi asubuhi nataka mtaro huu uwe msafi wananchi wasipatwe na magonjwa ya mlupuko" alisema Bonah
Katika ziara hiyo Kata ya Kimanga leo Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli alishirikiana na viongozi wa kata Kimanga wakiongozwa na Diwani wa Viti Maalum Rukia Mwenge na viongozi wa chama.
Katika ziara hiyo Mbunge Bonnah alikagua Eneo la kujenga zahanati eneo la soko ,kivuko cha watembea kwa miguu mtaa Twiga na matundu ya vyoo na baadae mkutano mkubwa wa Wananchi.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo Abdalah Lumungwi alisema wananchi wa eneo hilo wamekuwa wazito katika suala la utunzaji Mazingira
Post A Comment: