Serikali imeyataka makampuni ya simu za mkononi kutumia fursa ya mkongo wa Taifa kupeleka huduma za mawasiliano maeneo ya vijijini, ili kufikia azma ya serikali ya kuhakikisha huduma ya mawasiliano inaimarika kote nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknlojia ya Habari, (Mb) mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akiwa kwenye ziara ya kwanza ya kuyatembelea Makampuni yote ya simu ili kuweza kufahamu jinsi huduma zinavyowafikia wananchi na maeneo ambayo hajafikiwa na huduma za mawasiliano yaweze kupata huduma.

Katika ziara hiyo Mhandisi Mahundi ametembelea  vitengo vyote muhimu vya kampuni ya simu ya mkononi ya  Vodacom ikiwemo huduma kwa wateja ambapo ameweza kuona jinsi wananchi wanaendelea kutafutiwa suluhu katika changamoto ambazo wanazipata katika mawasiliano.

“Timu ya wakurugenzi wa vodacom mmenipitisha kwenye vitengo vyote muhimu kazi nzuri sana lakini kubwa nilihitaji kujionea zaidi kwenye eneo la huduma kwa wateja ambapo tumeona namna gani wananchi wameweza kutafutiwa suluhu ya changamoto zote ambazo zinaendelea kujitokeza lakini mpaka sasa nyingi zimeweza kupungua kwasababu wananchi wamepungua katika kuleta matatizo”amesema Mhandisi Mahundi .

Akielezea zaidi Mhandisi Mahundi amesema changamoto nyingi zimepungua kutokana na njia mbali mbali kuelekezwa kwa wananchi ili kuona kwamba zinatatuliwa kwa haraka kwani kuna zingine za kuongea na watoa huduma moja kwa moja na zingine kuwa kidigital zaidi ambapo wananchi wanaweza kupata huduma hizo.

Kwa hiyo siku ya leo nimeweza kupita hapa Vodacom na kujionea mitambo ya kisasa na namna gani wameweza kuiboresha kwa hiyo nitapita Makampuni yote ya watoa huduma kwa lengo la kuona kwamba eneo la utoaji huduma lote linakaa vizuri na kuwasisitiza kufika yale maeneo ambayo bado huduma ya mawasiliano inasuasua na mtandao kupatikana kwa shida maeneo hayo ambayo zaidi ni vijijini.

Share To:

Post A Comment: