NAIBU Waziri wa habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi(Mb), Maryprisca Mahundi amewataka watanzania kuacha kutoa taarifa zao binafsi kwenye mitandao  ya kijamii kwani duniani imeharibika.

Amesema wao kama viongozi wanaendelea kufanya wajibu wa kuhakikisha wanathibiti tabia hizo  ambazo zimekuwa zikifanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Mhandisi Mahundi amesema hayo Julai 12,2024  wakati akizungumza na wanafunzi wa chuo kikuu cha Katoliki cha CUom kilichopo Jijini Mbeya.

"Mimi  na wewe lazima tuthibiti pamoja tunza taarifa zako usimpe mtu yeyote na usimwamini  mtu  leo  mpo  kwenye urafiki kesho mkikosana amezipeleka harafu inakuja kuleta shida"amesema Mhandisi Mahundi.

Aidha Mhandisi Mahundi amesema wao  kama  wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari miezi miwili iliyopita Rais Samia alizindua Taasisi ya kutunza taarifa za mtu binafsi lakini bado kuna watu watukutu mtaani wa kukopesha fedha ndogo ndogo kuanzia sh.100,000 kushuka chini mtu akichelewa kulipa zinaanza kutumiwa jumbe za vitisho kwa watu waliopo kwenye Simu ya mkopaji .

"Pametokea ombwe kubwa sana mitaani la kukopesha fedha ndogo ndogo mkopaji akichelewa tu wale watu waliopo kwenye Simu ya mkopaji wanaanza kutumiwa sms za vitisho kuwa bwana David alikopa kiasi Fulani cha fedha na kuwa wewe ni mmoja wa wadhamini wake sababu tu mnawasiliana mara kwa mara na wakati huo David anakopa hakukuwa na mawasiliano yeyote na hivyo mwisho wa siku unakuta unapigwa picha bila kujijua"amesema Mhandisi Mahundi.

Akielezea zaidi Mhandisi Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya pia amesema kwamba wizara ya Habari Mawasiliano Teknolojia ya Habari wanashirikiana na jeshi la polisi kupitia Kitengo cha "Cirber" kushughulikia changamoto hiyo kwa kutoa matangazo kwa wananchi kuwa makini na taarifa zao binafsi kuacha kutoa ovyo.

"Huko mnako cheza cheza kwenye mitandao ya kijamii msiweke taarifa zenu binafsi na msipende kuandika  onyo mfano Facebook, Twitter, Instagram na mitandao mingine ya kijamii Dunia imeharibika hivi Sasa umakini  ni muhimu "amesema.

Baadhi ya wanachuo walioshiriki mkutano huo wamesema kuwa mitandao ya kijamii imekuwa changamoto kubwa na baadhi ya vitendo vya  udhalilishaji vimekuwa vikipitia  huko .

Share To:

Post A Comment: