HALMASHAURI ya Arusha wilayani Arumeru imefanikiwa kutekeleza miradi 40 ya Maendeleo ya Jamii chini ya mfuko wa TASAF, yenye thamani ya bilioni2.3 ikiwe miradi ya ujenzi wa shuleni na kituo Cha Afya.


Akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Selemani Msumi amesema miradi hiyo imefanyika katika vijiji 16 katika halmashauri hiyo na wamefanikiwa kupata miradi 40 ya uboreshaji wa miundombinu ya elimu na afya ikiwemo miradi kuendeleza miundombinu katika Kijiji Cha oldonyowas katika sekondari ya oldonyowas na mradi wa ujenzi wa kituo Cha Afya Bwawani," amesema.

Msumi, amesema katika Kijiji cha Oldonyowas chenye Sekondari ya Oldonyowas umetekelezwa jumla ya miradi 11 yenye thamani ya zaidi ya milioni 920.

Ametaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa mawili, ofisi mbili, choo cha matundu manne na samani, ujenzi wa nyumba mbili za walimu, ujenzi wa jengo la utawala, ujenzi wa mabweni SITA ya wavulana na wanaume, ujenzi wa maabara ya jiografia na fizikia na ujenzi wa uzio.

"Kituo Cha Afya Bwawani kimepata jumla ya milioni 611.125 kwaajili ya kutekeleza miradi nane ya miundombinu ya Afya ambayo ni ujenzi wa majengo ya wagonjwa wa nje kata za Bwawani na majengo, ujenzi wa jengo la mama na mtoto kata ya mwandeti, na kata ya Lamelock, ujenzi wa maabara kigongoni, ujenzi jengo la upasuaji Namagana na Songambele na ujenzi wa nyumba ya watumishi 3 kwa 1," amesema.

Amesema miradi hiyo imeleta manufaa makubwa kwa jamii ikiwemo kuongezeka kwa miundombinu ya elimu na afya, kuongeza ufanisi wa waalimu kufanyakazi kufuatia kuwepo maeneo ya shule.

Msumi amesema pia faida nyingine ni kuchangia kupata matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani yao, jamii kupata mafunzo ya usimamizi na uendeshaji wa miradi midogo midogo ya kuwaongezea kipato, huduma za Afya kupatikana kwa Karibu na huduma za maji, umeme kusogezwa Karibu.

Hata hivyo amesema miongoni mwa changamoto walizopata ni pamoja na mfumuko wa bei ambao umesababisha gharama za mradi kuongezeka wakati wa utekelezaji pamoja na wananchi kushindwa kuchangia kulingana na asilimia zinazotakiwa kutokana na kipato kidogo kinachotegemea kilimo.

Amesema ili kukabiliana na changamoto hizo, Halmashauri imeendelea kuhamasisha jamii kuchangia zaidi ili kukamilisha miradi sambamba na kushirikisha wadau mbalimbali.
Share To:

Post A Comment: