Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Ndugu Mohammed Ali Kawaida (MCC) amewasihi Viongozi wa UVCCM Mikoa na Wilaya zote nchi nzima walioshiriki kwenye Mafunzo katika Chuo cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Ihemi mkoani Iringa kwenda kuishi kwenye misingi ya Uongozi kwa Vitendo huku wakizingatia Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama Cha Mapinduzi. 

Ndugu Kawaida ameyasema hayo alipokua anahutubia Viongozi na Watendaji wa UVCCM katika Ufungaji wa mafunzo ya Viongozi na Watendaji wa UVCCM Mikoa na Wilaya zote nchi nzima yaliyofanyika Ihemi Mkoani Iringa kuanzia tarehe 11 Julai, 2024 hadi tarehe 17 Julai 2024. 

"Ndugu zangu wote hapa mmepata mafunzo yanayostahili tuna amini yanakwenda kurahisisha utendaji kazi wenu katika Maeneo yenu, niwasihi sana nendeni mkaishi katika misingi ya Uongozi kwa kuzingatia Katiba, Kanuni na Miongozo ya Chama chetu". 

"Nimefurahishwa sana namna ambavyo mmekua wasikivu, mmeishi kwa ushirikiano, mmeishi kwa Umoja na kuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo yenu, mmedhihirisha kuwa ninyi ni Viongozi wa kweli na mmekua katika misingi ya uongozi ndani ya CCM"






Share To:

Post A Comment: