Mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga kupitia kampuni yake ya Jahpeople amechangia zaidi ya shilingi milioni 490 kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya mbalimbali ya kimaendeleo katika sekta ya Elimu,Afya na ujenzi wa ofisi za serikali za mitaa na kata kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2021/2020- 2023/2024.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Makambako Keneth Haule katika mkutano wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama cha mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kwa kipindi cha miaka mitatu katika ukumbi wa Green City.
Haule amesema kila kata imepata fedha hizo kutoka kwenye kampuni ya Jahpeople, ambapo kata ya Makambako imepata milioni 33.5,Mjimwema milioni 16, Kivavi milioni 69, Kitisi milioni 25.7, Mwembetogwa milioni 34.7, Majengo milioni 18.9 Lyamkena milioni 47.5, Maguvani milioni 15,Mlowa milioni 17.5, Mahongole milioni 78, Kitandililo milioni 62.3, Utengule milioni 41.4.
Katika taarifa hiyo imebainisha kuwa miradi ya kimaendeleo yenye thamani ya zaidi ya bilioni 14.1 imetekeleza katika Halmashauri ya mji wa Makambako wilayani Njombe kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo bilioni 11 zimetokana na serikali kuu, bilioni 2.1 mapato ya ndani ya Halmashauri na wadau mbalimbali ikiwemo michango ya Wananchi, madiwani na Mbunge ni bilioni 1.2.
Post A Comment: