G32A0255


Mbunge wa Viti Maalum ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe.  Ummy Nderiananga amewataka viongozi wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), kwa kushirikiana na viongozi wa Chama kuhamasisha watu wenye ulemavu kushiriki katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Mhe. Nderiananga alitoa kauli hiyo tarehe 27 Julai 2024 wakati alipozungumza na viongozi wa UWT Kata katika Jimbo la Same Magharibi  katika  mkutano wa hadhara mara baada ya kutembelea Tarafa ya Chome Suji na Same, Kata ya Makanya na Tarafa ya Mwembe Mbaga iliyopo Kata ya Mwembe ambapo alisema kwa sasa Serikali imeweka mazingira rafiki kwa watu wenye ulemavu  kujiandikisha na kuboresha taarifa zao .

1000362310

“Viongozi wa Chama na Jumuiya zake tunao wajibu mkubwa wa kuhamasisha watu wenye ulemavu kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura na kwa sasa tumeboresha sana ili kuendana na hali zao hivyo niwaombe msisite kujitokeza kujiandikisha,” alisema Naibu Waziri Ummy.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba watu wenye ulemavu kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa pamoja na uchaguzi mkuu  unaotarajiwa kufanyika mwaka 2025 huku akiwataka viongozi wa CCM kuunga mkono kundi hilo akisema lina mchango mkubwa katika maendeleo.

1000362307

Mhe. Nderiananga alieleza kwamba, Wilaya ya Same ni ngome ya Chama cha Mapinduzi hivyo akawataka  wanaccm pamoja na Wananchi kutokukubali kuchezewa na viongozi wa vyama vya upinzani na kuwasihi kushiriki kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kupigia kura ili kupata fursa ya kutetea Wilaya ya Same ili kuendelea kuwa ngome ya CCM.

“Natambua bado zoezi la kujiandikisha katika daftari la kupigia kura halijafika Kilimanjaro lakini niwaombe viongozi wa chama changu endeleeni kuhamasisha wananchi ili pindi muda utakapofika washiriki kwa wingi kujiandikisha na kuwachagua viongozi wanaotokana na CCM,” alisisitiza.


Kwa upande wake, Katibu wa UWT Mkoa wa Kilimanjaro, Irimina Mushongi aliwahimiza  wanawake kuhakikisha wanamchagua Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumpa kura za kishindo katika uchaguzi mkuu mwakani. 

Katibu huyo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wakinamama kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuwachagua viongozi bora watakaowavusha katika maendeleo.
1000362301
1000362303
Share To:

Post A Comment: